BOLTON, England
KIUNGO Fabrice Muamba alirejea Bolton usiku huu na kumwaga machozi mbele ya mashabiki baada ya kipindi kisichopungua wiki sita tangu apatwe matatizo ya moyo uwanjani na kuzimia.
Kiungo huyo alitinga uwanjani wakati wa mechi ya Ligi Kuu England kati ya timu yake, Bolton dhidi ya Tottenham, timu aliyocheza nayo katika Kombe la FA wakati anazimia Mach 17.
Akionekana mwenye afya tele na bashasha, Muamba alitokwas machozi wakati akisalimia mashabiki kwenye Uwanja wa Reebok.
'natamani ningecheza leo,''alisema Muamba.
Baada ya kusalimia umati wa mashabiki, Muamba alielekea jukwaani kuishangilia timu yake.
Mapigo ya moyo ya Muamba yalisimama kwa dakika 78, Machi 17, lakini tiba makini aliyopatiwa na wataalamu wa moyo iliokoa maisha yake.
Aliruhusiwa kutoka hospitali ya London Chest, Aprili 16.
'Hii ni sehemu maalum: sapoti imekuwa kubwa na ninafurahia hilo,'' Muamba alisema. ''Niko sawa. Nazidi kuimarika kila siku. nafurahi kurudi, nina furaha kuweza kuzungumza na watu tena na kutembea mwenyewe.
0 comments:
Post a Comment