Barton kulia akizunguana na Tevez anayeamuliwa na wachezaji wenzake wa Man City |
NAHODHA wa QPR, Joey Barton amefungiwa mechi 12 na Chama cha
Soka England kwa vurugu alizofanya kwenye mechi dhidi ya Manchester City katika
siku ya mwisho ya msimu huu wa Ligi Kuu.
Barton ameongezewa adhabu ya mechi nane katika mechi nne za
awali sambamba na kutozwa faini ya pauni 75,000.
Aligombana na Sergio Aguero na Vincent Kompany, lakini baada
ya kupewa kadi nyekundu akamuanzishia na Carlos Tevez, na baadaye akawazingua
marefa.
Pamoja na hayo hajaadhibiwa kwa kwa kumsukumia kichwa
Kompany, Tume Kanuni imesema katika taarifa kwa kitendo alichomfanyia Sergio
Aguero anastahili adhabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment