Jabu kushoto akitafuta mbonu za kumtoka Elmiro Lobo wa Msumbiji, katika mechi ya kwanza ya kuwania tiketi ya AFCON mwakani, iliyofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Februari 29, 2012. |
Mratibu wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser ameiambia BIN ZUBEIRY machama huu katika mahojiajno maalum, ofisini kwake, barabara ya Nyerere, Dar es Salaam, kwamba Jabu ameongeza mkataba wa miaka mitatu Manungu.
"Kuna timu zinamfuatilia Javu, zikidhani amemaliza mkataba ili zimsajili bure, ni kwamba amekwishaongeza mkataba,"alisema Bayser.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu 1999 na 2000, walimpandisha kijana huyo kutoka timu yao ya vijana chini ya umri wa miaka 20 msimu uliopita na sasa amekuwa tishio kwenye Ligi Kuu, huku Simba, Azam na Mtibwa zikimmezea mate.
Javu tayari anaelekea kuwa na namna ya kudumu kwenye kikosi cha Stars, ingawa kwa sasa mara nyingi hutokea benchi akiwapokea akina Mbwana Samatta na John Bocco 'Adebayor', ambao kwa sasa ndio 'top strikers' bongo.
0 comments:
Post a Comment