Washiriki Miss Tabata 2012 |
SHINDANO la kumsaka mrembo wa Tabata, Miss Tabata 2012,
litafanyika Juni 1 katika ukumbi wa Da West Park, Tabata.
Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema kuwa onyesho
hilo pia kutakuwa na sherehe kabambe ya kusherehekea miaka 10 ya Miss Tabata.
“Shindano la mwaka huu litakuwa ni la aina yake kwa sasabu
hii itakuwa ni mwaka wetu wa 10 kuanda Miss Tabata. Tutakuwa na burudani nyingi
kutoka nje na ndani ya nchi. Pia tutahakikisha tunashirikisha warembo bomba
wenye hadhi ya kushinda taji la Miss World,” Kapinga alisema mratibu huyo wa
Bob Entertainment na Keen Arts.
Kapinga alisema kuwa warembo waliyowahi kushinda mataji
tofauti tofauti la shindano hilo pia watakuepo kusherekea miaka 10 ya Miss
Tabata.
Warembo watakaoshiriki kwenye shindano wanaendelea na
mazoezi kila siku katika ukumbi wa Dar West Park.
Warembo hao ni Neema Saleh (18), Noella Michael (19), Queen
Issa (20), Hycalisa Joseph (18), Phillios Lemi (19), Wikllihemina Mvungi (20)
na Nightness Rajab (19). Wengine ni Suzanne Pancras (19), Caroline David (21),
Khadija Nurdin (19), Jamila Omary (18), Advent
Mamkwe (21), Nadya Marjeby (21), Axer Peter (20), Rahama Hassan (19),
Mercy Mlay (21) na Diana Simon Laizer (20).
Kapinga aliwaomba warembo wenye sifa kuendelea kujitokeza
waweze kupata wawakilishi bora katika shindano la Kanda ya Ilala.
"Bado milango iko wazi, mrembo yoyote anayejiamini
kwamba ana vigezo anakaribishwa. Tunataka shindano la mwaka huu liwe na
ushindani zaidi,” mratibu huyo aliongeza.
Warembo 10 watachaguliwa kushiriki mashindano ya Miss Ilala
na baadaye Miss Tanzania.
Mrembo anayeshikilia taji la Tabata ni Faiza Ally.
Warembo wa Tabata wamekuwa wakifanya vizuri katika
mashindano ya Miss Tanzania ambapo mwaka juzi Consolata Lukosi alishinda nafasi
ya tatu kabla ya kutangazwa kuwa balozi wa kinywaji cha Redds. Katika shindano
la mwaka juzi Julliet William pia alishinda nafasi ya tatu katika ngazi hiyo ya
taifa.
Juliet ndiye anayeshikilia taji la dunia la Miss Progressive
International.
0 comments:
Post a Comment