SHINDANO la Miss Dar Inter College 2012 linatarajiwa
kufanyika Juni 8, mwaka huu katika ukumbi wa San Sirro, Sinza, Dar es Salaam likisindikizwa
na burudani baab kubwa, kutoka kwa wasanii na vikundi ambavyo vitatajwa baadaye,
kwa mujibu wa Dina Ismail, Mratibu wa shindano hilo.
Vimwana 15 wanaendelea na mazoezi, chini ya mwalimu wao, Marylidya
Boniphace, Miss Dar Inter College 2009 kwenye hoteli ya Lamada, Ilala mjini Dar
es Salaam.
BIN ZUBEIRY ilitembelea kambi ya warembo hao jioni ya leo, na
kukuta totoz zisizopungua nane zikijinoa, wakati warembo wengine walikuwa wana
udhuru. Hebu cheki totoz na jiulize kwa njini Juni 8 usiende San Sirro kucheki
swaga zao.
|
0 comments:
Post a Comment