Bin Kleb akimkabidhi jezi Haruna Niyonzima baada ya kumsajili mwaka jana mjini Kigali 'kwa bei chafu' kutoka APR ya Rwanda |
MDAU wa soka nchini, Abdallah Ahmed Bin Kleb ameomba ijitokeze
kampuni ya kuwadhamini marefa wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, ili
kuwawezesha kujimudu na kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY usiku huu, Bin Kleb
aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, kabla ya kujiuzulu alisema
kwamba marefa wa Tanzania wanafanya kazi katika mazingira magumu na wanalipwa
posho kidogo mno na TFF.
“Nasikia wanalipwa Sh. 70,000, hizi ni fedha kidogo sana,
haziwezi kuwatosheleza kujikimu, naomba ijitokeza kampuni maalum, kwa ajili ya
kuwadhamini marefa wa Ligi Kuu, kwa sababu kwa kufanya hivyo kampuni zitanufaika
kwa sababu watatangazwa kibiashara,”alisema.
Bin Kleb alisema kwamba, wakati mwingine watu wanakosea
kuwatupia shutuma nyingi waamuzi kwamba wanapenda rushwa, ingawa hutokea hatakwa
waamuzi walio waadilifu wakaingia kwenye
mitego kwa sababu ya hali halisi inayowakabili.
Aidha, Bin Kleb alisema anastaajabishwa mno na vyombo vya
habari nchini, kuelekeza nguvu zao katika mechi za Ligi Kuu zinazochezwa Dar es
Salaam pekee, wakati mikoani ndiko kuna mambo mengi ‘ya ajabu’.
“Unakuta Televisheni zinaonyesha mechi za Dar es Salaam
pekee, wakati huko mikoani ndiko kuna mambo ya ajabu kweli kweli, ambayo
yanatakiwa yaripotiwe ili yakomeshwe, kwa hivyo natoa haya mawili kama
changamoto kwa maslahi ya soka yetu,”alisema Bin Kleb.
0 comments:
Post a Comment