Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Geroge Kavishe akizungumza na Waandishi wa Habari leo wakati akitambulisha kampeni ya 100% tz Flava leo katika hoteli ya New Africa. |
UCHUNGUZI uliofanywa na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George
Kavishe umemuonyeaha mambo mawili makubwa kuhusu Tanzania- kwanza ni muziki wa
nchini kuwa bidhaa inayonunuliwa zaidi nje na pili Simba na Yanga kuwa kwenye
tano ya wapinzani wa jadi jadi dunaini.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya 100% TZ
Flava, iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa mchana huu mjini Dar es Salaam,
Kavishe alisema kwamba mbali na Simba na Yanga kuwa kwenye tano bora ya
wapinzani wa jadi duniani, pia zinashika nafasi ya pili Afrika.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Executive Solutions, waratibu wa kampeni ya 100% tz Flava akizungumza na Waandishi wa Habari katika hoteli ya New Afrika leo |
Akiizungumzia kampeni hiyo, Kavishe alisema kwamba itatembea
kwa miezi sita na itapambwa na mambo mengi mazuri ya kujivunia kuhusu Tanzania.
Alisema kampeni hiyo itakuwa na sehemu tatu, ambayo ni kwanza
kuzindua alama ya kampeni hiyo, 100% tz Flava- tusherehekee kilicho chetu.
“Kwenye hii kampeni, imetengenezwa ili kumpa mteja raha, lakini
lazima iache ujumbe, ambao ni furahia kilicho chetu. Kampeni inahusu muziki wetu, tumetumia picha
za wanamuziki wetu,”alisema Kavishe na kuongeza;
“Kwanza nataka niwaambie kama mlikuwa hamjui, bidhaa ambayo inauzika
nje zaidi kwa sasa hapa Tanzania, ni muziki wetu, watu wa nje ya nchi wananunua
sana muziki wetu na ndio bidhaa inayoongoza kuuzika nje ya nchi,”alisema.
Alisema pia wametumia picha za Simba na Yanga, klabu ambazo zinadhaminiwa
na bia hiyo. “Hakuna nchi duniani, klabu zake za ndani zina ukubwa na uzito
ambao Simba na Yanga zinao. Mvuto wa Simba na Yanga duniani ni wa tano kwa
ukubwa. Na kwa Afrika wa pili,”alisema Kavishe.
Aidha, Kavishe pia alisema katika kampeni hizo, pia wametumia
lugha za mtaani, ambazo pia ni fahari ya Tanzania kwa mfano piga tarumbeta, neno
linalowakilisha kunywa bia kwa kutumia chupa moja kwa moja na kula bata, yaani
kula raha.
Mapema, Kavishe alisema kampeni hii ni mwendelezo wa kampeni
ya Kili Jivunie Utanzania, ambayo amesema kwa kiasi kikubwa imefanikiwa.
“Bia ya Kilimanjaro Lager ipo tangu mwaka 1954. Ilipotea wakati
wa harakati za uhuru na ikarudi mwaka 1966
kama Kilimanjaro Premium Lager na hadi leo tunasukumana nayo, tunabadilisha nembo
na kadhalika, lakini bado tupo nayo,”alisema.
Kavishe alisema bia kama maisha ya mwanadamu, inazaliwa, inakuwa,
inakomaa na inakufa- lakini kudumu kwa bidhaa sokoni kunatokana na kampeni
inayofanywa kuibakiza sokoni.
Alisema uchunguzi walioufanya mwaka 2009 ili kutambua kwa nini
bia ya Kilimanjaro ipo sokoni na wateja wanaionaje, uliwaonyesha kwamba bia
hiyo inakubalika mno mbele ya Watanzania.
Waandishi wakisikiliza kwa makini |
“Sisi tulikuwa tunajua ni Safari Lager, tukataka kujua bia
ipi inakubalika zaidi kama ya Kitanzania, majibu yaliyokuja hatukukubaliana
nayo. Hatukuamini, walisema ni Kilimanjaro Premium Lager,” alisema.
Kavishe alisema Safari Lager iko sokoni tangu mwaka 1977 na
ilikuwa inachukuliwa kama ni bia ambayo asili yake ni Tanzania kutokana na
alama ya kanyumba ka msonge, lakini wateja wao wakasema ni Kilimanjaro kwa
sababu ya alama ya mlima Kilimanjaro, mnyama Twiga na kufanya vitu ambavyo
vinawagusa Watanzania moja kwa moja.
0 comments:
Post a Comment