Salha Israel, Miss Tanzania 2011 |
KAMPUNI ya Lino International Agency, waandaaji wa Miss Tanzania, imewataka warembo wanaotaka kushindana
katika shindano dogo la kumsaka mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya
Dunia (Miss World 2012) wameombwa kuendelea kuchukua fomu za kushindana katika
kinyang’anyiro hicho na kuzirudisha kabla ya Juni 4.
Mkurugenzi wa Lino
International Agency, Hashim Lundenga ameiambia BIN ZUBEIRY jioni hii kwamba sema kuwa wanatarajia kufanya mchujo wa washiriki
Juni 5 kwa ajili ya kubakiza warembo 10 kwa ajili ya kuwania nafasi ya
kushiriki katika mashindano ya Dunia yaliyopangwa kufanyika Agosti 18 kwenye
ukumbi wa Dongsheng Fitness Center Stadium,
mjini Ordos, Inner Mongolia, China.
Lundenga alisema kuwa zoezi hilo lilisimamishwa kutokana na zuio la
Serikali na wakati huo, jumla ya warembo
12 walikuwa wamekwisha chukua fomu za kushiriki. Alisema kuwa muda wa kufanya
mashindano hayo umekaribia na wanatarajia kuitangaza tarehe mpya hivi karibuni.
Alisema kuwa amefurahishwa na
kasi ya kuchukua na kurejesha fomu, hata hivyo wanahitaji warembo wengi zaidi
ili kuweza kupata wigo mpana kwa ajili ya kumsaka mrembo atakayewania taji la
Dunia ambalo kwa sasa lina mikononi mwa mrembo kutoka Venezuela, Ivian Sarcos.
“Tunakaribia kufanya
mashindano madogo hivi karibuni, hivyo ni wajibu wetu kuwakumbusha warembo
wanaotaka kuwania taji hilo kufanya hivyo kabla ya Juni 4 ili kuweza kuingia
katika zoezi la mchujo,” alisema Lundenga.
Alisema kuwa mpaka sasa jumla
ya nchi 84 zimekwisha pata wawakilishi wao kwa ajili ya mashindano hayo. Nchi
32 pamoja na Tanzania bado hazija chagua wawakilishi wao katika mashindano
hayo.
Fomu za kuomba kushiriki zinapatikana katika
ofisi za Miss Tanzania za jijini na mawakala wote wa mashindano hayo katika
mikoa ya Tanzania Bara.
0 comments:
Post a Comment