KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini amemuomba radhi kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson kwa kitendo ch mshambuliaji wake, Carlos Tevez kubeba bango la R.I.P. Fergie katika kusherehekea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya England jana.
Tevez alibeba bango hilo kubwa wakati wa sherehe za klabu ya City baada ya kushinda taji la ligi kuu nchini England.
Lakini kitendo hicho cha Tevez kinasaidikwa kuwa ni jibu kwa usema wa Ferguson aliotoa mwaka 2009 pale alipoulizwa kama kuna siku Manchester City itakuwa mbele ya timu yake Manchester United. Wakati huo mkufunzi Ferguson alijibu kwamba hilo haliwezi kufanyika wakati wa uhai wake.
Hata hivyo Tevez mwenyewe alisema baadaye kwamba haku-kusudia kumkosea heshima Sir Alex ferguson.
0 comments:
Post a Comment