Tetesi J'nne Magazeti ya Ulaya

MAN CITY HAITANII KWA VAN PERSIE, INAMTAKA KWELI...

MABINGWA wapya wa Ligi Kuu ya England, Manchester City wako kwenye nafasi nzuri ya kumsajili Nahodha wa Arsenal, Robin van Persie kwa dau la pauni Milioni 25, wakimuahidi mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki.
BAHATI iliyoje kwa Arsenal, mchezaji wao mpya, Lukas Podolski amesema kwamba atakuwa akicheza washambuliaji watatu katika nafasi moja katika kikosi cha washika Bunduki wa London msimu ujao.
Robin van Persie
Van Persie aliigharimu Arsenal pauni Milioni 2.75, akitokea Feyenoord ya Uholanzi mwaka 2004
KLABU ya Manchester United imeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Robert Lewandowski, baada ya mazungumzo yake na klabu yake juu ya mkataba mpya kufa. Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Poland, mwenye umri wa miaka 23, amefunga mabao 30 msimu huu.
KIUNGO wa Lille, Eden Hazard amesema kwamba atajiunga na klabu ya Manchester msimu huu. Hata hivyo, Mbelgiji huyo mwenye umri wa miaka 21 hakusema itakuwa ipi kati ya City au United.
KLABU za Chelsea na Liverpool zinaelekea kumkosa kiungo wa Sao Paolo ya Brazil, Lucas Moura, kutokana na Inter Milan kuonekana wameingia kwa gia kubwa zaidi katika vita ya kuwania saini ya kinda huyo Mbrazil mwenye umri wa miaka 19.
KLABU ya West Brom inabangua bongo kama imsajili moja kwa moja, kipa Ben Foster anayewadakia kwa mkopo au la. Mchezaji huyo Bora wa Mwaka wa The Baggies, anatarajiwa kurejea timu ya Daraja la Kwanza, Birmingham msimu huu.

DALGLISH OUT LIVERPOOL

KOCHA wa Liverpool, Kenny Dalglish amekwenda Boston kupambana kupigania ajira yake, kufuatia tetesi kwamba kocha wa  Wigan, Roberto Martinez anaweza kuchukua nafasi yake Anfield.
Roberto Martinez
Martinez 
Martinez nimtu anayetakiwa, na Aston Villa inaaminika kumuweka Mspanyola huyo na kocha wa Norwich, Paul Lambert katika orodha ya makocha inaowataka kurithi mikoba ya Alex McLeish iliyemfukuza.
     MARADONA
GWIJI wa Argentina, Diego Maradona amesema alifurahia taji la ubingwa wa Ligi Kuu England, ambalo walilitwaa Manchester City, akisema; "Kwa moyo wangu wote". Bao la ushindi la City dhidi ya QPR, lilifungwa mkwewe, Sergio Aguero aliyemuolea binti yake.