Tetesi za Ijumaa magazeti Ulaya

MAN CITY WAIPA FEDHA NA MCHEZAJI BARCELONA ILI WAMTWAE DANI ALVES

KLABU ya Manchester City inajiandaa kuchukua mchezaji mwingine Barcelona, beki nyota Dani Alves, mwenye umri wa miaka 29. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania, City wametoa ofa ya pauni Milioni 12 na kuwapa Aleksandar Kolarov pia.
MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Mario Balotelli ameonyesha nia yake ya kubaki katika klabu hiyo, akikanusha uvumi kwamba anataka kurejea Italia kujiunga na  AC Milan.
KLABU ya Manchester United inajiandaa kuboresha ofa yake ya ya pauni Milioni 13 kumnasa kiungo Shinji Kagawa mwenye umri wa miaka 23, kutoka Borussia Dortmund.
KLABU ya Tottenham ipo karibu kumsaini beki wa kati Jan Vertonghen, mwenye umri wa miaka 25, kutoka Ajax kwa dau la pauni Milioni 9.6.
KLABU ya Arsenal iko tayari kwa mazungumzo ya kumchukua mshambuliaji wa Montpellier, Olivier Giroud kwa ofa ya dau la pauni Milioni 6.4, pamoja na kuwapa Marouane Chamakh, ili wamnase mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25.

MWENYEKITI WIGAN AMUONYA MARTINEZ

MWENYEKITI wa Wigan, Dave Whelan amemtaka kocha wake, Roberto Martinez kufikiria kwa umakini juu ya kujiunga na  Liverpool kufanya kazi chini ya Mkurugenzi wa Soka.
KOCHA wa zamani wa England, Fabio Capello anakuwa kocha wa mwingine kusitisha mpango wa kwenda Liverpool, lakini bado ana matumaini ya kupata kazi Chelsea.
KOCHA Steve Bruce anatakiwa na Hull City akachukue nafasi ya Nick Barmby, lakini hawezi kuchukua uamuzi wowote kwa sasa, akiwa anavizia kurejea kwa mara ya tatu Wigan, iwapo Martinez ataondoka.
KOCHA wa Muda wa Chelsea, Roberto Di Matteo anatakiwa na klabu ya nyumbani kwao, Italia, Napoli baada ya mazungumzo yake na klabu yake ya sasa, Chelsea kuwa bado hayajafanyika.