NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mh. Amos Makalla
amesema amejitoa kwenye Kamati za Simba baada ya kuteuliwa kuwa Waziri na kuanzia
sasa atakuwa akisaidia klabu zote nchini.
Makalla amesema hayo katika sherehe za ubingwa wa Ligi Kuu
ya Bara za Simba kwenye ukumbi wa Dar Live, Mbagala jioni ya leo.
Pamoja na hayo, Makalla amesema amechangia sana mafanikio ya
Simba msimu huu, akiwa kwenye Kamati aliyoteuliwa na ameutaka uongozi wa klabu hiyo
kutobweteka na mafanikio hayo na badala yake kujipanga vizuri ili kufanya
vizuri zaidi.
0 comments:
Post a Comment