BAO la kujifunga la Martin Skrtel dakika ya tano usiku huu, limeipa Fulham ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Anfield dhidi ya Liverpool inayojiandaa na fainali ya Kombe la FA.
Katika mchezo huo, Liverpool ilishindwa kuendeleza wimbi la ushindi ililoanzisha Jumamosi iliyopita, ilipoichapa 3-0 Norwich.
Na kipigo hicho kinamaanisha timu ya Kenny Dalglish imeendelea kuboronga ikiwa imeshinda mechi tatu tu za Likgi Kuu kati ya mechi 13 zilizopita.
Liverpool inabaki kuwa imeshinda mechi tano tu msimu huu kwenye Uwanja wa Anfield msimu huu, wakati Fulham, ambayo imezinduka kutoka kwenye kipigo cha 4-0 kutoka kwa Everton mwishoni mwa wiki iliyopita, sasa imefikisha pointi sawa na wenyeji wao, 49.
Sasa kuna hatari ya Wekundu hao kumaliza nje ya Nane Bora kwa mara ya kwanza msimu huu, tangu 1954, waliposhuka daraja.
Ikiwa na mabadiliko ya wachezaji tisa kutoka kikosi kilichoifunga Norwich Jumamosi, ilikuwa dhahiri Dalglish alichemka. Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo usiku huu, Stoke City imetoka 1-1 na Everton nyumbani.
VIKOSI, KADI (0) & WALIOINGIA NA KUTOKA (3)
Liverpool
- 32 Doni
- 06 Aurelio (Jose Enrique - 65' )
- 16 Coates
- 34 Kelly
- 37 Skrtel
- 11 Maxi
- 14 Henderson (Downing - 46' )
- 20 Spearing
- 33 Shelvey
- 09 Carroll
- 18 Kuyt
BENCHI
- 01 Jones
- 03 Jose Enrique
- 23 Carragher
- 38 Flanagan
- 49 Robinson
- 19 Downing
- 31 Raheem Sterling
Fulham
- 01 Schwarzer
- 02 Kelly
- 03 JA Riise
- 05 Hangeland
- 18 Hughes
- 13 Murphy
- 16 Duff
- 23 Dempsey
- 31 Kacaniklic (Frei - 58' )
- 07 Pogrebniak
- 30 Dembele
BENCHI
- 12 Stockdale
- 06 Baird
- 28 Briggs
- 10 Kasami
- 20 Etuhu
- 21 Frei
- 09 Sa
Refa: Probert
Mahudhurio: 40,106
0 comments:
Post a Comment