MICHUANO ya Ligi ya Taifa inayoshirikisha mabingwa wa mikoa
inaanza Mei 27 mwaka huu katika vituo vitatu tofauti huku Ashanti United ya
Ilala na Polisi ya Mara zikifungua dimba katika Kituo cha Musoma.
Ligi hiyo ambayo inatarajia kumalizika Juni 12 na 13 mwaka
huu itashuhudia mechi mbili kwa siku katika kila kituo, huku ya kwanza
ikichezwa saa 8 mchana na kufuatiwa nay a pili 10 jioni.
Mechi za ufunguzi Kituo cha Musoma ambapo mechi zake
zitachezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma ni Flamingo ya Arusha
dhidi ya Forest ya Kilimanjaro (saa 8 mchana) wakati saa 10 jioni ni Ashanti
United na Polisi.
Kituo cha Kigoma siku ya ufunguzi kutakuwa na mechi moja tu
itakayoanza saa 10 kamili jioni kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika kati ya Mwadui
ya Shinyanga na JKT Kanembwa ya Kigoma. Siku inayofuata ni CDA (Dodoma) vs
Majimaji ya Tabora (saa 8 mchana) na Bandari ya Kagera vs Pamba ya Mwanza (saa
10 kamili jioni).
Tenende ya Mbeya na Kurugenzi ya Iringa ndizo zitakazoanza
saa 8 mchana kwenye Kituo cha Mtwara na kufuatia na mechi kati ya Mpanda Stars
ya Rukwa na Ndani ya Mtwara kuanzia saa 10 kamili jioni. Mechi hizo zitachezwa
katika Uwanja wa Umoja.
0 comments:
Post a Comment