George Kavishe, Meneja wa Kilimanjaro Beer |
Gaudence Mwaikimba, mfungaji bora wa taifa Cup msimu uliopita akiwa na mabingwa watetezi Mbeya |
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana usiku katika
mahojiano maalum, Nyumbani Lounge, Oysterbay, Dar es Salaam, Kavishe alisema
kwamba Kilimanjaro Premium Lager bado ni wadhamini wa Taifa Cup na mwaka huu
itafanyika kama kawaida.
Hata hivyo, alipoulizwa juu ya ukimya wa maandalizi hadi
sasa, Kavishe alisema; “Sisi tunawasubiri TFF (Shirikisho la Soka Tanzania),
wao ndio wanatakiwa kutupa mwongozo, sisi ni wadhamini tu, tunawezesha, ila
mipango yote na nini, ni TFF wao wenyewe,”alisema Kavishe ambaye jana bia yake
ilifanya pati la uzinduzi wa kampeni ya Kilimanjaro Premium Lager 100% TZ Flava
kwenye ukumni wa Nyumbani Lounge.
Kumekuwa na wasiwasi wa Kombe la Taifa ama kutofanyika
kabisa mwaka huu, au kufanyika bila ya udhamini, baada ya Kilimanjaro Premium
Lager ambao pia ni wadhamini wa klabu za Simba na Yanga, kuingia mkataba wa
kuidhamini Taifa Stars, ambayo awali ilikuwa inadhamini na bia ya Serengeti
Premium Lager.
Lakini kauli hii ya Kavishe inakuja kuondoa wasiwasi huo na
mikoa sasa inaweza kuendelea na maandalizi yake kama kawaida.
0 comments:
Post a Comment