MAHAKAMA Kuu yaTanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imepanga Juni 11 mwaka huu kuendelea kusikiliza ushahidi wa upande wa Jamhuri wa kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (TBF), Shaabani Mintanga ya kusafirisha dawa za kulevya kilo 4.8. Kwa mujibu wa shajala ya Mahakama, kesi hiyo itaendelea kusikilizwa siku hiyo mbele ya Jaji Dk. Fauz Twaib, ambaye alikuwa akiisikiliza tangu mwanzo. Kesi hiyo iko katika hatua ya kusikilizwa mashahidi wa upande wa Jamhuri, ambapo mashahidi ambao wameshatoa ushahidi ni pamoja na Godfrey Mroso ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Anvelope Travel Agency, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) , Charles Ulaya na kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya ngumi, Nassoro Michael. Mintanga alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwaka 2008, akikabiliwa na mashitaka ya kula njama na kusafirisha dawa za kulevya kilo 4.8.
Lookman crowned African footballer of the year
-
The 2024 Confederation of African Football (CAF) Award took center stage on
Monday night, with the best talents in African football emerging winners.
The...
Edozie Njoku and the new APGA
-
By Ambrose Ododo it has been a long and tortuous journey for the birth of
the rebranded All Progressives Grand Alliance, APGA, and it looks like it
is go...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment