Yondan kulia katika mechi na TP Mazembe mwaka jana |
YANGA waandike maumivu. Hawampati ng’o Kelvin
Yondan- labda hadi 2015.
Hiyo inafuatia, Makamu Mwenyekiti wa Simba,
Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ kuiambia BIN ZUBEIRY mchana huu kwamba beki huyo wa
kati amesaini mkataba mpya wa miaka miwili.
“Yondani alikwishasaini muda mrefu tu,
kipindi kile amegoma na kubaki kwao Mwanza, ishu ilikuwa fedha, alikuwa anataka
fedha, sisi tukamuita tukampa fedha, akamwaga wino,”alisema Kaburu.
Aidha, Kaburu alisema kwamba Victor Costa
ana nafasi ya kumalizia mkataba wake wa mwaka mmoja SImba SC, iwapo atajirekebnisha
na kurudi akiwa fiti Juni mwaka huu.
“Tumevunja kambi, baadhi ya wachezaji
wanakwenda kambi ya timu ya taifa, lakini wengine ambao hawana majukumu kipindi
hiki tumewaambia wakajitunze, wakirudi wawe fiti.
Kila mtu kapewa programu ya kufanya mazoezi
angalau ya gym kila baada ya siku moja,”alisema Kaburu.
Yanga
imekuwa ikimtaka kwa mkuda mrefu Yondan, lakini kila kinapowadia kipindi cha
usajili hushindwa kumnasa katika mitego yao.
0 comments:
Post a Comment