Kaseja wa pili kutoka kulia katika kikosi cha Simba SC |
Simba imeaga michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Al Ahly Shandy, juzi Jumapili.
Mafisango na Kaseja ndio wacheza
ji waliokosa penalti Simba ilipofungwa kwa penalti 9-8 baada ya muda wa mchezo kumalizika kwa jumla ya mabao 3-3.
"Nilijiskia vibaya kukosa penalti sababu nilijua ilikuwa muhimu kwangu kwa timu, ila ni bahati mbaya, sijui nini kimetokea uwanjani, ni sehemu ya mchezo ila tulijiandaa kushinda na kila mmoja wetu alijua hivyo."
Gazeti la Mwanaspoti leo, limemnukuu Nahodha wa Simba, Juma Kaseja akisema kuwa walifungwa kutokana na kuvurugikiwa kisaikolojia baada ya wapinzani wao kurudisha mabao yote matatu ndani ya dakika 15 za kwanza za kipindi cha pili.
"Tulipoteana uwanjani, hakuna kati yetu aliamini kuwa wangeweza kusawazisha yale mabao. Kipindi cha kwanza tulicheza vizuri sana, ila ndani ya dakika tano za kipindi cha pili walifunga mabao mawili na la tatu hatukuamini," alisema Kaseja.
"Nina uzoefu na wachezaji wa Simba, baada ya kufungwa mabao matatu, niliwaangalia usoni na kuona wamebadilika." Alisema ndio maana ulipofika wakati wa penalti, wachezaji wenzake waliogopa kupiga kwa kuogopa lawama na wengi walikuwa wamepoteza morali.
"Nikiwa kama nahodha niliwalazimisha kupiga, kocha ananiuliza Kaseja nani anapiga, nikimtaja mtu anaogopa, ikabidi nitumie nguvu, sababu ilibidi tupige," alisema Kaseja.
"Walishinda kwa sababu penalti, siku zote hata kwa timu kubwa kama Real Madrid au Barcelona, haina mwenyewe ni kama kitu cha bahati, tucheza vizuri ila makosa madogo yalikuwa chanzo, ila kwa sasa tusilaumiane, tuangalie tulipojikwaa kwa ajili ya michuano ijayo," alisema.
Kaseja alidokeza kuwa uchovu kwa wachezaji wake ni kikwazo pia."Kwa muda mfupi tumecheza mechi nyingi na wachezaji ni wale wale tu, kama mabadiliko ni kidogo sana.
Kocha asilaumiwe kwa kuchezesha wachezaji wale wale kwa sababu anajaribu kutengeneza timu ya pamoja, iliyokaa kwa muda mrefu na kuelewana kama vile ilivyo kwa Manchester United na timu nyingine kubwa duniani."
"Najua wengi watashangaa kwa nini tumeweza kushinda nyumbani mabao 3-0 na kufungwa ugenini mabao kama hayo katika muda wa dakika 90 na baadaye kupoteza penalti, hii ni kawaida, kwani, kawa tuliweza kuwafunga nao pia inawezekana kwa upande wao, mpira hauna kanuni, tuliweza kuruka vizingiti na kushinda mengi ngumu na kupoteza kwa timu ya kawaida kama Al ahly shandy, huu ndio mpira,"alisema Kaseja kwa huzuni.
"Ni kweli, kwa mtazamo wangu, tunahitaji kusajili wachezaji mahiri, kutokana na upungufu tuliouona ila tusitumie kigezo cha kutolewa katika michuano ya Kombe la Shirikisho kama kigezo cha kuvuruga timu.
"Ili timu ielewane, inahitaji kukaa pamoja viongozi waangalie maeneo ambayo yanahitaji kuongezewa nguvu na kusajili wachezaji wazuri kwa ajili ya msimu ujao wa ligi na michuano ya klabu bingwa ya Afrika itakayokuja mbele yetu, majina hayachezi uwanjani, tuangalie uwezo wa wachezaji katika kuisaidia timu ishinde na kufanya vizuri."
Ushindi huo wa Shandy ambao haukutegemewa kwa wenyeji kutokana na kuwa na uzoefu mdogo katika michezo ya kimataifa na hofu yao kwa Simba, umesogeza timu hiyo hatua ya 16 bora
0 comments:
Post a Comment