![]() |
Kaseja akilia, akibembelezwa na Machaku |
KIPA wa Simba, Juma Kaseja jioni hii ameshindwa kujizuia
lilipotajwa jina la Patrick Mafisango kwenye sherehe za ubingwa wa Ligi Kuu ya
klabu hiyo na kujikuta akimwaga machozi kwenye ukumbi wa Dar Live, Mbagala, Dar
es Salaam.
Kaseja alimwaga machozi wakati alipokuwa akipokea Medali kwa
niaba ya marehemu Mafisango, aliyefariki dunia wiki iliyopita kwa ajali ya gari
maeneo ya Keko, Dar es Salaam, kabla ya kuzikwa kwao, DRC siku tatu baadaye.
Kiungo wa Simba, Salum Machaku aliitoa Medali aliyokabidhiwa
kwenye sherehe hizo kwa marehemu Mafisango.
Kaseja, ambaye pia ni Nahodha wa Simba, alinyamaza baada ya
kubembelezwa na wachezaji wenzake na kuendelea na shughuli hiyo iliyofana na
kuhudhuriwa na mamia ya wapenzi wa klabu hiyo.
Ukumbi pamoja na mapambano yake yaliyowekwa, lakini
ulipendeza zaidi kwa mavazi ya mashabiki wa Simba ya rangi nyekundu na nyeupe.
Meneja wa Global Publishers Limited, Abdallah Mrisho
alikabidhi Sh. Milioni 3 kwa Kaseja kama zawadi yao kwa Simba kutokana na
kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.
Baada ya yote hayo,
wachezaji na viongozi wa Simba walifungua shampeni na sherehe ikaanza rasmi-
kwa hakika mambo yalikuwa mazuri Dar Live, bendi ya Msongo Ngoma ikianza
kutumbuiza, ikiongozwa na mwimbaji wake mkongwe, shabiki maarufu wa Simba, Mzee
Muhiddin Mwalimu Gurumo.
0 comments:
Post a Comment