![]() |
Wachezaji mazoeini jioni ya leo, Uwanja wa Amaan jioni ya jana |
KAMBI ya timu ya taifa ya Zanzibar, inayojiandaa na michuano
ya Kombe la dunia kwa nchi zisizo wanachama wa FIFA (Shirikisho la Soka la
Kimataifa), inakabiliwa na hali ngumu mno na zaidi inaendelea kwa sababu ya uzalendo
wa wachezaji pekee.
BIN ZUBEIRY jana imetembelea kambi hiyo visiwani hapa na kufanya
mahojiano na Kocha Mkuu, Ahmad Morocco, ambaye amesema kama si uzalendo wa
wachezaji, basi safari ya Uzbekistan kwenye mashindano hayo yanayoanza Juni 4, mwaka
huu ingekufa.
Morocco amesema vijana wapo kambini Bwawani Hotel, lakini
hata chakula ni cha matatizo. “Hawapati chakula cha kutosha, yaani wanapewa
chakula kwa kiwango ambacho wamepanga wenye hoteli, si lishe ya kula mchezaji,
lakini tutafanyeje na hiyo ndio hali halisi,”amesema Morocco.
CHANZO CHA MATATIZO:
![]() |
Nikiwa kwenye mazungumzo na kocha Morocco |
“Wao wanasubiri matokeo mabaya waje kulaumu tu, lakini
katika hali kama hii, ukifanya vizuri basi unastahili sifa sana, mimi nakuambia
hata dawa tu hapa ni tatizo, timu haina dawa wala nini,”amesema.
Morocco anasikitika kwamba hata wachezaji wa timu hiyo wapo
kambini kwa zaidi ya siku 10, lakini hawapati posho na anaamini Chama cha Soka
Zanzibar (ZFA) hakina uwezo kwa sababu hakina wafadhili zaidi ya kutegemea
serikali.
“ZFA wanasema wamekwishapeleka bajeti yao Wizarani, lakini
ajabu hadi sasa wanasema hawajajibiwa chochote, na hali inazidi kuwa mbaya kambini,
maana yake wachezaji wanatumia chao cha mfukoni hadi wanaishiwa, sasa hata
familia zao watazisaidiaje,”amesema.
SMZ IMEISUSA TIMU?
![]() |
Selembe kushoto na Gulam kulia wakijiandaa kuingia mazoezini |
PAMOJA NA YOTE, VIJANA UZALENDO MBELE:
![]() |
Abdi Kassim kushoto na Abdulhalim Humud kulia wakipasha |
Morocco amesema timu itaondoka Juni 2, kupitia Dar es Salaam
tayari kwa mchezo wa kwanza dhidi ya Tehran na anasema kwa ujumla wamepania kurejea
na Kombe hilo. “Sisi kwa pamoja, azma yetu ni kurejea na Kombe, ili tuwadhihirishie
wananchi wa Zanzibar uzalendo wetu,”amesema.
SABRI, FAROUK WATEMWA SAFARINI, CANNAVARO CHUPUCHUPU
![]() |
Cannavaro na mkewa wakiwa jukwaani wanaangalia mazoezi |
Bado kikosini watakuwepo wachezaji wengine hodari tu
wakiongozwa na nyota wa Azam FC, viungo Abdi Kassim ‘Babbi’, Abdulhalim Humud ‘Gaucho’,
Suleiman Kassim ‘Selembe’, beki wa Yanga, Cannavaro, ambaye naye chupuchupu
akose safari kutokana na majeruhi na mshambuliaji wa Canal Suez ya Misri, Ally
Badru.
Cannavaro ameshindwa kufanya mazoezi leo kutokana na
kufanyiwa upasuaji mdogo wa jipu kwenye goti, lakini daktari wa timu amethibitisha
anaendelea vizuri na kesho ataaanza tena mazoezi.
Katika kikosi hicho atakosekana pia beki Aggrey Morris Ambroce,
ambaye yuko kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars
kinachokwenda kucheza na Ivory Coast mwishoni mwa wiki, kikiondoka alfajiri ya
kesho Dar es Salaam.
Morocco amesema pengo la Morris limezibwa vema na beki Salum
Tall anayecheza soka ya kulipwa Oman, ambaye alicheza soka nzuri mno katika mechi
ya kujipima nguvu na Malawi jana iliyoisha kwa sare ya 1-1. Malawi pia ilicheza
na Taifa Stars Jumamosi wakatoka 0-0.
0 comments:
Post a Comment