GWIJI wa soka, Johan Cruyff amemaliza utata kuhusu wanasoka wawili bora zaidi duniani kwa sasa, akisema mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi ni mzuri zaidi ya mshambuliaji wa Real Madrid, zote za Hispania, Cristiano Ronaldo, kwa sababu "ana mapenzi na mpira."
Washambuliaji hao wawili, wanalingana kwa mabao katika La Liga, 43 kila mmoja wakifukuzana kuwania tuzo ya kiatu cha dhahabu maarufu kama Pichichi na wachambuzi wengi wanasema ni vigumu kwatenganisha nyota hao wawili kwa vipaji vyao.
Pamoja na hayo, Cruyff anafikiri nyota wa Blaugrana, ambaye ameshinda tuzo ya Ballon d'Or kwa miaka mitatu iliyopita, bado mdogo.
"Messi au Cristiano?" Mholanzi huyo aliulizwa katika mahojiano na Cadena COPE, akasema:. "Messi, kwa sababu ana mapenzi na mpira. Ni fundi mtupu na mtoto mzuri."
Wakati huo huo, kocha huyo wa zamani wa Barca, amemuunga mkono kocha wa sasa wa klabu hiyo, Pep Guardiola kwa uamuzi wake wa kuachia ngazi baada ya kuitumikia klabu kwa miaka minne.
"Guardiola amefanya kitu sahihi," alisema babu huyo mwenye umri wa miaka 65-. "Atarudi siku moja, lakini sijui kama atakuwa kama kocha."
Guardiola alikuwa mchezaji katika kikosi hatari cha Cruyff, 'Dream Team', ambacho kilitwaa mataji manne mfululizo Hispania miaka ya 1990, sambamba na kuipa Barca Kombe la kwanza la Ulaya.

0 comments:
Post a Comment