KOCHA wa Italia, Cesare Prandelli ametaja orodha ya mwisho
ya wachezaji 23 kwa ajili ya UEFA EURO 2012 saa chache kabla ya mechi ya
kirafiki na Luxembourg mjini Parma, huku beki Andrea Ranocchia na mshambuliaji
Mattia Destro wakiwa wachezaji wa mwisho kuiacha kambi ya The Azzurri.
Baada ya kupunguza wachezaji kutoka 32 hadi 25 jana, huku
kipa Francesco Viviano, mabeki Davide Astori, Salvatore Bocchetti, Domenico
Criscito na viungo Luca Cigarini, Ezequiel Schelotto na Marco Verratti akiwatema,
Prandelli ametaja kikosi chake cha mwisho katika siku ya mwisho ya kuwasilisha
orodha ya wachezaji kwa ajili ya michuano hiyo.
Nyota mwenye umri wa miaka 24, Ranocchia aliyepitia msimu
mgumu kwa kuandamwa na majeruhi akiwa na FC Inter Milan na kinda wa miaka 21,
Destro kwa mastaajabu ya wengi wameorodheshwa kikosini. Kinda huyo, Destro
amefunga mabao 12 msimu huu Serie A akiwa na AC Siena.
KIKOSI KAMILI ITALI;
Makipa; Gianluigi Buffon (Juventus), Morgan De Sanctis (SSC
Napoli), Salvatore Sirigu (Paris Saint-Germain FC).
Mabeki: Ignazio Abate (AC Milan), Federico Balzaretti (US
Città di Palermo), Andrea Barzagli (Juventus), Leonardo Bonucci (Juventus),
Giorgio Chiellini (Juventus), Christian Maggio (SSC Napoli), Angelo Ogbonna
(Torino FC).
Viungo: Daniele De Rossi (AS Roma), Alessandro Diamanti
(Bologna FC), Emanuele Giaccherini (Juventus) Claudio Marchisio (Juventus),
Riccardo Montolivo (ACF Fiorentina), Thiago Motta (Paris Saint-Germain FC),
Antonio Nocerino (AC Milan), Andrea Pirlo (Juventus).
Washambuliaji: Mario Balotelli (Manchester City FC), Fabio
Borini (AS Roma), Antonio Cassano (AC Milan), Antonio Di Natale (Udinese
Calcio), Sebastian Giovinco (FC Parma)
Cesare Prandelli has named his final 23-man squad for the EURO©Getty Images
0 comments:
Post a Comment