KOCHA Roy Hodgson ameanza kuiongoza timu ya taifa ya England vyema, kwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Norway, katika uwanja wa Ullevaal mjini Oslo jana.
Kabla ya mechi hiyo, England ilikuwa imeshindwa kuishinda Norway katika kipindi cha miaka 32 iliyopita.
Ashley Young ndiye aliyefunga bao hilo la pekee katika mechi hiyo, katika dakika za mwanzomwanzo za mechi hiyo ya kirafiki.
Hodgson alipata nafasi nzuri ya kuwatizama wachezaji wa England ambao ataweza kuwashirikisha zaidi katika juhudi zake za kuisuka vyema timu yake itakayoshiriki katika mashindano ya Ulaya ya Euro 2012, baada ya kuchukua kazi hiyo kutoka kwa Fabio Capello.
Timu ya England ilionyesha nidhamu ya hali ya juu na anayoitazamia Hodgson, lakini wengi bila shaka wanafahamu timu ambayo England itakutana nayo, Ufaransa, tarehe 11 mwezi Juni katika mji wa Donetsk, haitacheza sawa na timu waliyopambana nayo mjini Oslo.
Lakini yalikuwa ni mazoezi ya kuridhisha kwa Hodgson, ambaye sasa ataweza kukinoa kikosi chake vyema zaidi katika mechi nyingine ya kirafiki katika uwanja wa nyumbani wa Wembley, Jumamosi ya tarehe 2 Juni, wakati England itakapoikaribisha timu ya taifa ya Ubelgiji
0 comments:
Post a Comment