NIKIWA mwandishi wa muda mrefu,
niliyelelewa katika misingi na maadili ya kitaaluma, napenda kuwaambia wasomaji
wangu kwamba, sitoi kipaumbele kwa habari za migogoro kwenye blog yangu.
Nasikitika, sitakuwa naandika habari yoyote
ya mgogoro- nikiamini kabisa wakati umefika Watanzania tunapaswa kubadilika na
kuachana na desturi hiyo, badala yake kufikiria namna ya kujiletea maendeleo.
Lazima tukubali kukabiliana na changamoto-
kwa kufuata misingi ya sheria na katiba- badala ya kuweka mbele vurugu na uvunjaji
wa sheria.
Kwa sababu hiyo, tunaanzia na huu mgogoro
wa Yanga unaoendelea hivi sasa, BIN ZUBEIRY haitaupa nafasi. Sera kubwa ya BIN
ZUBEIRY ni kuandika habari za maendeleo, kuelimisha na kuburudisha wasomaji
wake.
Siwezi kuingilia uhuru wa blogs nyingine-
au magazeti hata Radio na Televisheni, lakini kwangu narejea kwenye mafundisho
na uzoefu nilioupitia chini ya magwiji wa taaluma ya Habari nchini, nikiwa
mfanyakazi wa kampuni ya Habari Corporation (sasa Neww Habari) tangu 1998 hadi
nilipoacha kazi Mei 1, mwaka huuu.
Nasema, BIN ZUBEIRY ni kwa habari za
maendeleo, na si migogoro. Asanteni. Mungu ibariki Tanzania, bariki sekta yetu
ya michezo, iwe na amani mafanikio. Amin.
0 comments:
Post a Comment