// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); HII NDIYO DAWA YA TIBA YA MGOGORO JANGWANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE HII NDIYO DAWA YA TIBA YA MGOGORO JANGWANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, May 01, 2012

    HII NDIYO DAWA YA TIBA YA MGOGORO JANGWANI


    Yanga fanyeni mkutano mkuu kuinusuru klabu Send to a friend
    Monday, 30 April 2012 14:31
    BARAZA la Wazee la Yanga limetangaza kuichukua timu hiyo, huku likitoa sababu tatu ambazo zimewafanya kuichukua timu hiyo.

    Sababu hizo ni kupoteza ubingwa, klabu kukosa uwezo wa kifedha wa kuisafirisha timu katika mechi mbalimbali za Ligi Kuu na timu yao kupata mapato kidogo katika mechi wanazocheza.

    Juzi Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga alisema, Yanga ilikuwa na kikao cha Kamati ya Utendaji kwa ajili ya kujadili suala hilo la Baraza la Wazee la Yanga kuamua kuichukua timu ya Yanga.

    Tunaamini uamuzi utakaotoka katika kikao hicho utakuwa wa manufaa kwa timu hiyo kwa sababu bila hivyo tunaona utaibuka mgogoro ambao utaiathiri timu ya Yanga.

    Ni wazi suala la Baraza hilo la Wazee la Yanga kuichukua timu hiyo siyo halali kwa mujibu wa sheria za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa sababu kuna mkutano halali wa klabu hiyo unaoweza kufanya mabadiliko ya uongozi wa klabu.

    Hivi karibuni baada ya Yanga kupoteza matumaini ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu, baadhi ya wanachama wa klabu ya Yanga walianza kuonekana kukasirishwa na hali hiyo, hivyo kuanza kuwataka viongozi wa ngazi ya juu wa Yanga kujiuzulu.

    Sisi hatuwezi kuzuia mawazo ya watu, ila tunaona ni muhimu kwa wanachama wa Yanga kutulia katika kipindi hiki na kushughulikia matatizo yao bila mgogoro huku wakizingatia mwisho wa ligi hii ndiyo mwanzo wa maandalizi ya Ligi Kuu nyingine.

    Tunasema hivyo kwa sababu kupata na kukosa zote ni hali, kama wamekosa ubingwa msimu huu wanaweza kutumia muda wao vizuri katika kipindi cha mwisho wa ligi kufanya usajili mzuri wa wachezaji na kuanza maandalizi mapema kwa ajili ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu msimu ujao.

    Tunapenda kuwasihi wanachama wa Yanga watambue kwamba zipo sababu sababu tatu za msingi zinazofanya soka la Tanzania lisiendelee ambazo ni migogoro, ukosefu wa fedha na kukosekana kwa programu maalumu za kuendeleza mchezo wa soka.

    Tunasema hivyo kwa sababu tumekuwa tukishuhudia migogoro katika vyama vyama vya soka nchini, pia tumeshuhudia migogoro ikijitokeza katika klabu za soka na kuwaathiri wachezaji kwa kiasi kikubwa.

    Migogoro hii imekuwa ikidumaza soka la Tanzania na kusababisha timu zetu kufanya vibaya katika mashindano ya kimataifa kwa sababu imekuwa ikiwahusisha viongozi na kuchukua muda mwingi kuishughulikia kuliko kuandaa timu zetu za soka au kutafuta wadhamini wa kusaidia kudhamini programu za soka.

    Wote tunafahamu hakuna mdhamini atakayekubali kuweka fedha zake sehemu ambayo ina migogoro kwa sababu kwa namna moja au nyingine naye atahusika katika mgogoro ule. Hivyo kusababisha hata wadhamini hao kushindwa kufanya biashara zao na makampuni mengine kwa sababu tayari naye ni sehemu ya mgogoro.

    Tunafahamu wanachama wa Yanga wana haki ya kuhoji utendaji wa viongozi wao, lakini tunaamini wanao utaratibu waliojiwekea wa kufanya hivyo pamoja na kuwawajibisha  kama wanaona hawafai badala ya kuanzisha mgogoro.

    Tunaamini wanachama wa Yanga wanaelewa hawawezi kupata malaika wa kuongoza klabu hiyo kwa kuwa viongozi wao hutoka miongoni mwao wanachama wa Yanga, ambapo kama tunavyofahamu hakuna binadamu asiye na makosa.

    Hatusemi Uongozi wa Yanga hauna makosa au una makosa ila tunaamini zipo taarifa zinazoandaliwa na viongozi wao waliopo madarakani ambazo huwakilishwa katika mkutano halali wa klabu hiyo unaotakiwa kufanyika kila mwaka.

    Tunaamini katika mkutano huo wanachama huwa na nguvu kubwa ya kuhoji mambo mbalimbali ambayo wanaona siyo sahihi katika kuhakikisha klabu yao inafanya vizuri.

    Tunapenda kuwashauri wanachama wa Yanga wakumbuke kuwa kila mara wanapopata nafasi adhimu ya kuchagua viongozi wao wawe wanatumia vizuri nafasi hiyo kuliko wanavyofanya sasa wanawachagua viongozi halafu wanawapindua.

    Ili kujinusuru na mgogoro mkubwa unaoweza kutokea ni bora viongozi wa Yanga wakaitisha mkutano mkuu wa klabu hiyo haraka iwezekanavyo na kupanga mikakati ya kutatua matatizo yao.

    GAZETI LA MWANANCHI:
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HII NDIYO DAWA YA TIBA YA MGOGORO JANGWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top