KIKAO cha Kamati ya Utendaji ya Yanga kujadili barua ya
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Wakili Lloyd Baharagu Nchunga kujiuzulu kimeshindwa
kufanyika leo, kutokana na safu kutotimia.
Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesigwa ameiambia BIN
ZUBEIRY mchana huu kwamba, Mbaraka Igangula yupo Afrika Kusini wakati
Khalifa Mgonja yupo Arusha,
Mwesigwa alisema kwa sababu hiyo, wanasubiri Wajumbe wote wa
Kamati ya Utendaji wafike Dar es Salaam ndipo kikao kifanyike. Wakati huo huo,
Wazee wa klabu hiyo walikutana na waandishi wa Habari leo mchana makao makuu ya
klabu na kusema kwamba, hawamtambui Mjumbe yeyote wa Kamati ya Utendaji, kwani
Nchunga ameondoka na watu wake wote.
Aidha, baadhi ya Wajumbe waliotangaza kujiuzulu wameanza
kuzikana barua zao, wakidai walilazimika kuandika kutokana na vitisho
walivyokuwa wakipewa. BIN ZUBEIRY
iliwasiliana na Mwanasheria wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alex
Mgongolwa kutaka ufafanuzi zaidi juu ya sakata la klabu hiyo, lakini akasema
yuko kwenye kikao.
Wakati BIN ZUBEIRY ikiwa imetega rada zake kwa Mgongolwa
hadi hapo atakapomaliza kikao, taarifa zaidi zinasema kikao hicho kinahnusu
syala hilo hilo la Yanga na atalitolea tamko leo.
Jana, Nchunga alitangaza kujiuzulu Uenyekiti wa Yanga,
akisema timu anaikabidhi kwa Baraza la Wadhamini, ambalo kwa sasa linaundwa na
wajumbe watatu, Mama Fatuma Karume, Deo Filikunjombe na Francis Kifukwe.
0 comments:
Post a Comment