SIMBA TUNU YA AFRIKA MASHARIKI
SASA ni rasmi kwamba Simba SC ndiyo fahari ya nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mwaka huu.
Kwa mujibu wa tovuti ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Simba ndiyo timu pekee ya Afrika Mashariki ambayo imebaki katika michuano ya makombe yanayosimamiwa na Shirikisho hilo.
Kwa mujibu wa tovuti hiyo, hakuna timu kutoka katika jumuiya hiyo ambayo bado ipo katika michuano hiyo ukiondoa Simba SC. Nchi tano zinaunda Jumuiya hiyo ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
Orodha hiyo inaonyesha kwamba nchi ya Sudan ndiyo kinara kwa ngazi ya vilabu barani Afrika kufikia sasa baada ya kuingiza timu nne katika michuano ya Ligi ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la CAF.
Timu ambazo Sudan imeingiza katika michuano hiyo ni El Merreikh na Al Hilal ambazo zimesonga mbele katika Ligi ya Mabingwa na Al Ahly Shandy na El Amal ambazo zimesonga mbele katika Kombe la Shirikisho (CAF).
Simba iliifunga 3-0 Al Ahly Shandy 3-0 katika mechi ya kwanza hatua ya 16 Bora Jumapili na sasa inahitaji sare au kufungwa si zaidi ya mabao 2-0 wiki ijayo ili kusonga mbele.
TOVUTI YA SIMBA SC
0 comments:
Post a Comment