Fergie na Giggs |
Wawili hao wa Manchester United walishinda tuzo hizo katika sherehe za miaka 20 ya Ligi Kuu.
Giggs ni mchezaji babu kubwa zaidi Man United, wakati Fergie ameshinda mataji 12 tangu aanze kazi mwaka 1986.
Nyota wa zamani wa Old Trafford, Gary Neville alisema: “Ryan Giggs atakuwa mchezaji Muingereza mwenye mafanikio ya muda mrefu na siwezi kumuona yeyote mmoja wa kumpiku.
Alan Shearer, kwa mabao yake 260, amejishindia tuzo ya mfungaji wa miaka 20 ya uhai wa ligi hiyo, wakati David James alipokea tuzo ya kipa aliyesimama langoni muda mrefu bila kuruhusu nyavu kutikiswa (173).
Neville, Giggs na Shearer pia walitajwa kwenye kombaini ya kikosi cha miaka 20 ya uhai wa Ligi Kuu.
KIKOSI CHA MIAKA 20 YA LIGI KUU:
Schmeichel (Man U), G Neville (Man U), T Adams (Arsenal), R Ferdinand (Man U), A Cole (Man U), Ronaldo(Man U), Scholes (Man U), R Keane (Man U), Giggs(Man U), Henry(Arsenal), Shearer (Newcastle).
0 comments:
Post a Comment