ENGLAND imetaja kikosi chake cha awali kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, mwaka huu huku kocha Roy Hodgson akimpa cheo cha Unahodha wa timu, kiungo wa Liverpool, Steven Gerrard.
John Terry, ambaye pia amejumuishwa kikosini, alivuliwa Unahodha wa timu Februari, uamuzi ambao ulimfanya aliyekuwa kocha wa Three Lions, Fabio Capello ajiuzulu.
Gerrard amewahi kuwa Nahodha wa England katika mechi 15, ya kwanza ikiwa dhidi ya Sweden, Machi mwaka 2004 na mechi ya karibuni kabisa ni dhidi ya Uswisi Septemba 2010.
Hodgson aliwaambia Waandishi wa Habari kwamb: "Kwa maoni yangu [Gerrard] ni mtu ambaye anaweza kumudu heshima hii,"alisema.
England itakuwa na mechi mbili za kujipima nguvu kabla ya Euro 2012, ambako Gerrard anatarajiwa kukiongoza kikosi kipya.
Mechi hizo za kirafiki ni dhidi ya Norway na Ubelgiji, kabla hya England kufungua dimba na Ufaransa Juni 11, 2012.

KIKOSI KAMILI THREE LIONS:
JINA | KLABU |
MAKIPA: | |
Joe Hart | Manchester City |
Robert Green | West Ham |
John Ruddy | Norwich City |
MABEKI: | |
Leighton Baines | Everton |
Gary Cahill | Chelsea |
Ashley Cole | Chelsea |
Glen Johnson | Liverpool |
Phil Jones | Manchester United |
Joleon Lescott | Manchester City |
John Terry | Chelsea |
VIUNGO: | |
Gareth Barry | Manchester City |
Stewart Downing | Liverpool |
Steven Gerrard | Liverpool |
Frank Lampard | Chelsea |
James Milner | Manchester City |
Alex Oxlade-Chamberlain | Arsenal |
Scott Parker | Tottenham |
Theo Walcott | Arsenal |
Ashley Young | Manchester United |
WASHAMBULIAJI: | |
Andy Carroll | Liverpool |
Wayne Rooney | Manchester United |
Danny Welbeck | Manchester United |
Jermain Defoe | Tottenham |
0 comments:
Post a Comment