Published: 34 minutes ago
NYOTA wa Chelsea, Didier Drogba aliwavutia maelfu ya mashabiki leo alipokuwa amebeba mwenge wa Olimpiki eneo la Swindon.
Drogba, ambaye alitangaza jana kubwaga manyanga Chelsea, aliwapungia mkono mashabiki wakati akiingia mjini na mwenge huo.
Wengi kati ya waliojitokeza kumuona shujaa wao wa kandanda, walikuwa wamevalia jezi za Chelsea.
Usiku huu, mwenge wa Olimpiki utamaliza mbio zake mikononi mwa Zara Phillips.
Mjukuu huyo wa kike wa Malkia,atakuwa nyuma ya farasi kubeba mwenge huo kuupeleka Cheltenham, kikomo cha mbio hizo maarufu.
Drogba, ambaye alikuwa mtu wa 84 kuushika mwenge huo leo, alipita barabara ya Commercial Road mjini Swindon katika eneo la maduka.
Barabara hiyo iligeuka kuwa bahari ya bluu, nyekundu na nyeupe kutokana na maelfu ya bendera, maputo na fulana za mashabiki wa soka.
Misururu pia ilijipanga katika mitaa ya Royal Wootton Bassett katika siku ya tano ya mbio hizo.
Katikati ya Jiji sherehe zilikuwa kubwa mno na maelfu walijimwaga.
Shangwe kubwa ilikwedna kwa kijana Ben Fox, mwenye umri wa miaka 16, ambaye amepania kushiriki Olimpiki ya walemavu, maarufu kama Paralimpiki ya mwaka 2016.
Chipukizi huyo anayecheza mpira wa kikapu wa walemavu, alilazimika kubadilisha mikono mnara kadhaa wakati akiubeba mwenge huo, lakini alifanikiwa kumaliza kiwango chake cha kuukimbiza mwenge huo.
0 comments:
Post a Comment