Drogba kushoto, Torres na Lampard kulia |
KOCHA wa Chelsea, Roberto Di Matteo anaweza kuwapanga pamoja katika safu ya ushambuliaji Fernando Torres na Didier Drogba wacheze pasha kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumamosi wiki hii, baada ya kuwajaribu wawili hao katika mechi na Blackburn Rovers mwishoni mwa wiki.
Wapachika mabao hao wawili, hawajawahi kuanza pamoja chini ya Mtaliano huyo katika kipindi chake cha miezi miwili ya kuwa kazini na kocha huyo wa zamani wa West Brom amesema atawaweka pamoja Jumamosi dhidi ya Bayern Munich Uwanja wa Allianz Arena.
"Nimejaribu vitu vichache ili kuwa mtazamo mpya na kuona itafanyaje kazi. Wakati wote ni ngumu, kwa sababu ni wazi itakuwa nafasi tofauti," alisema. "Lakini nimekuwa nikijaribu kubadilisha vitu vichache."
Wawili hao wote wamejaribu kuzinduka mwishoni mwa msimu na wote wamefunga mabao muhimu katika mechi ngumu, Drogba alifunga kwenye fainali ya Kombe la FA wakati Torres alifunga bao la dakika za mwishoni Uwanja wa Camp Nou lililoipeleka The Blues fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Huku viungo Ramires na Raul Meireles ikifahamika wataikosa mechi hiyo, Di Matteo anaweza kabisa kuimarisha kikosi chake kuwa mpanga Drogba na Torres mbele.

0 comments:
Post a Comment