13 Mei, 2012 - Saa 17:35 GMT
MSHAMBULIAJI Alessandro del Piero aliwaaga kwa Kibibi Kizee cha Turin, akifunga bao lake la mwisho katika mechi ya mwisho kuichezea Juventus kama bingwa mpya wa Ligi ya Sere A baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Atalanta jana.
Juventus imehitimisha msimu wa Ligi ya Italia bila kushindwa hata mara moja na Del Piero alihitimisha kwa magoli mawili kumalizia kipimdi cha miaka 20 akiichezea klabu hio.
Ulikua wakati wa hisia za majonzi kwenye uwanja wa San Siro ambakoKlabu ya AC Milan iliwaaga wakongwe wa mchezo wa soka Alessandro Nesta, Gennaro Gattuso na Filippo Inzaghi pamoja na Mark van Bommel.
Inzaghi alifunga bao kuisaidi Milan katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Novara. Hata hivyo ushindi huo haukuwa na maana yoyote kwa sababu Juventus tayari ilikua inaongoza kwa pointi 4 kabla ya mechi ya mwisho na kujishindia Ligi ya msimu ikiwa ni ushindi wa mara 28.
Mji wa Turin ulikua katika hali ya sherehe ambapo maelfu ya mashabiki walimiminika mitaani kushereheka ushindi wa kwanza baada ya miaka 9.
Mjini Geneva matokeo ya jumapili FC Zürich 0 Servette 1, Thun 2 Young Boys 2, na jumamosi Basel 6 Grasshoppers 3, Lucerne 3 Lausanne-Sport 2.
Kwa matokeo hayo Salzburg ilijishindia Ligi ya Austria kwa mara ya 7 kwa mabao 5-1 katika mechi yao ya mwisho kwenye uwanja wa Wiener Neustadt
0 comments:
Post a Comment