Published: Today at 13:38
CHELSEA imewapokea tena wachezaji wake wawili waliokuwa majeruhi, hizi zikiwa habari njema kwa mashabiki wake kuelekea fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mjini Munich.
David Luiz na Gary Cahill, ambao wamekuwa nje ya Uwanja kwa maumivu ya nyama za paja, leo walifanya mazoezi na The Blues.
Kocha Roberto Di Matteo anahitaji mno beki, kutokana na John Terry na Branislav Ivanovic wote kufungiwa kucheza mechi hiyo.
Florent Malouda pia anasumbuliwa na nyama za paja.
Lakini Di Matteo alisema: “Flo, anaendelea vizuri na anatarajiwa kuwapo Jumamosi.”
0 comments:
Post a Comment