EXCLUSIVE
By Wayne Veysey | Chief Correspondent
By Wayne Veysey | Chief Correspondent
KLABU ya Chelsea, iko tayari kumpa ofa ya mkataba mpya
Ashley Cole ambao utamuweka Stamford Bridge kwa kipindi chote kilchobaki cha maisha
yake ya soka.
Beki huyo amebakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake wa
sasa na klabu hiyo inataka kumfunga kwa mkataba mpya mwanzoni mwa msimu ujao,
kwa mazungumzo ambayo yataanza hivi karibuni, baada ya beki huyo wa kushoto
kuonyesha soka ya nguvu msimu huu, akitoa mchango mkubwa kwa timu kutwaa taji
la Ligi ya Mabingwa.
Chanzo cha habari, kimeiambia Goal.com, ambako BIN
ZUBEIRY imeipata habari hii, kwamba beki huyo mwenye umri wa miaka 31
atapewa mkataba wa makia mitatu na kuingia kwenye orodha ya wachezaji
wanaolipwa vizuri katika klabu hiyo, sambamba na akina John Terry, Frank Lampard na Fernando Torres.
Mshahara wake wa sasa inasemekana ni kiasi cha pauni 120,000
kwa wiki, wakati Barcelona ni miongoni mwa klabu ambazo zinamtaka sana Cole na
kwa sasa inasikilizia tu kama Chelsea itashindwana naye, iingie msituni kusaka
saini ya mchezaji huyo, aliyesajiliwa Stamford Bridge katika mazingira ya utatanishi
kutoka Arsenal mwaka 2006.
Hadi sasa hakuna dalili kwamba Cole anataka kuondoka London
na baada ya kumaliza msimu na mataji mawili, kwa sasa yuko likizo Los Angeles, Marekani
kabla ya kujiunga na timu ya taifa ya England wiki ijayo kujiandaa na mchezo wa
kirafiki dhidi ya Ubelgiji Juni 2, mwaka huu.
Pamoja na kurefusha maisha ya Cole, Stamford Bridge, pia Chelsea
inataka kuwaongezea mikataba Michael Essien, Florent Malouda na Frank Lampard, ambao
wanamaliza 2013.
Kama BIN ZUBEIRY ilivyoinukuu Goal.com Jumatano kwamba Salomon
Kalou anaweza kutemwa, sasa suala lake litatatuliwa wiki ijayo, wakati Jose
Bosingwa anajiandaa kutemwa licha ya kuwa beki chaguo la kwanza kulia katika
kikosi kilichomaliza msimu na mataji mawili.
0 comments:
Post a Comment