John Bocco kushoto |
Bocco alitangaza kustaafu timu ya taifa, kwa sababu alikuwa walikuwa wanamzomea anapokosa mabao ya wazi naye akafikiri anapigwa vita vita kwa sababu hatokei Simba au Yanga.
Hata hivyo, baada ya wadai wengi wakiwemo viongozi wa TFF na serikali kumsihi awe mvumilivu na kurejea timu ya taifa, mfungaji huyo bora wa Ligi Kuu amekubali.
Habari kutoka TFF, zimesema kwamba kocha mpya wa Stars, Kim Poulsen aliwasiliana kwanza na Bocco kabla ya kumuita na amekubali.
Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 25 leo kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast. Akitangaza kikosi hicho ambacho kitaingia kambini kesho kutwa, miongoni mwao akiwa Bocco, Mchezaji Bora wa msimu wa washindi wa Medali ya Fedha Ligi kuu Bara.
Kim amesema uteuzi wake umezingatia uwezo wa mchezaji uwanjani, nafasi anayocheza na ubora wake. Wachezaji walioitwa ni makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally (Azam) na Deogratius Munishi (Mtibwa Sugar). Mabeki ni Nassor Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Simba), Waziri Salum (Azam), Shomari Kapombe (Simba) na Juma Nyoso (Simba). Viungo ni Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Abubakar (Azam), Nurdin Bakari (Yanga), Jonas Mkude (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Edward Christopher (Simba- U20), Mrisho Ngasa (Azam) na Frank Domayo (JKT Ruvu- U20). Washambuliaji ni Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Ramadhan Singano (Simba-U20), Simon Msuva (Moro United- U20), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Haruna Moshi (Simba) na John Bocco (Azam). Stars inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro itacheza mechi ya kirafiki nyumbani Mei 26 mwaka huu dhidi ya Malawi kabla kuivaa Ivory Coast ugenini Juni 2 mwaka huu jijini Abidjan.
0 comments:
Post a Comment