KLABU ya Barcelona imeripotiwa kumtayarishia kocha Tito Vilanova euro Milioni 100 kwa ajili ya kusajilia wachezaji wapya mwishoni mwa msimu.
Kwa mujibu wa jarida la Sport, The Blaugrana watapata euro Milioni 30 kutoka bajeti yao ya kawaida ya mwaka euro Milioni 50 ili kuimarisha kikosi chao. Pamoja na hayo, gazeti hilo limesema kwamba viongozi wa klabu hiyo wanaamini watatengeneza euro Milioni 30 nyingine kwa mauzo ya wachezaji.
Beki wa kulia, Dani Alves tayari amehusishwa na mpango wa kuhamia kwa mabilionea wa Urusi, Anzhi Makhachkala na inaaminika iko tayari kutoa mpunga mnene kumnasa Mbrazil huyo. Barca pia inatarajiwa kumuuza kiungo Seydou Keita mwishoni mwa msimu.
Pia kuna fedha ambazo kama timu ingetwaa taji la Ligi ya Mabingwa na La Liga ilikuwa ziende kwa wachezaji kama posho, sasa nazo zitaingia kwenye mfuko wa usajili.
Pia, kuondoka kwa kocha Pep Guardiola kutapunguza bajeti ya matumizi ya klabu kwani kocha aliyechukua nafasi yake, Tito Vilanova amekubali mshahara mdogo.
Kwa matokeo hayo, Barca wanaamini watakuwa na kitita cha euro Milioni 100 kufanyia usajili mwishoni mwa msimu, ili kujiimarisha mapema na kurejesha makali yake katikqa soka ya Ulaya.
Tayari Barca wanahusishwa na mpango wa kuwasajili mshambuliaji wa Athletic Bilbao, Fernando Llorente na beki wa pembeni wa Valencia, Jordi Alba.

0 comments:
Post a Comment