Published: Today at 12:53
MARIO Balotelli alipuuza pati la Manchester City kushangilia ubingwa wa Ligi Kuu England na kuamua kutoka kivyake usiku wa jana.
Mtaliano huyo alikataa kwenda pati la chakula cha usiku kilichoandaliwa maalum kwa pamoja na timu na kufanya mtoko kivyake na mdogo wake Enoch.
Kiwa amevaa kofia flat, mshambuliaji huyo alikwenda kwenye klabu la Kitaliano, San Carlo wakati wachezaji wenzake na kocha walienda kusherehekea ushindi wao unaokuja baada ya miaka 44 Hilton Hotel.
Hii si mara ya kwanza kwa Mario kupuuza sherehe za klabu baada ya ushindi mkubwa.
Mei mwaka jana alipuuzia sherehe za City baada ya kutwaa Kombe la FA.
Pia alishindwa kutokea kwenye sherehe za tuzo za msimu za klabu hiyo, zilizoambatana na chakula cha usiku, japo alishinda tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka.
0 comments:
Post a Comment