Chaz Baba kulia akimwambia Martine karibu sana. Kushoto ni King Dodo La Bouche, mwasisi wa Mashujaa Band |
Martine katikaqti, King Dodoo kulia na Chaz Baba kushoto katika utambulisho wa Meneja huyo mpya asubuhi hii |
MENEJA aliyefukuzwa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’,
Martine Sospeter leo ametangazwa rasmi kuwa Meneja mpya wa bendi ya Mashujaa-
ikiwa ni siku mbili tu afukuzwe katika bendi yake ya awali iliyompatia
umaarufu.
Martine, ametambulishwa asubuhi hii katika mgahawa wa Business
Park, Victoria, Dar es Salaam. Pamoja na utambulisho huo, Martine amekanusha madai
ya Mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka kwamba ametoweka na fedha za bendi
hiyo.
Katika taarifa yake ya kumfukuza kazi Martine, Asha alidai
Meneja huyo alichukua fedha kwa wateja kwa ajili kuwakodisha bendi- hivyo
akamtaka azirejeshe. “Sijachukua fedha yoyote popote, sina deni, kama anadai
nina deni, alete ushahidi,”alisema Martine.
Martine alisema kwamba kwa muda mrefu amekuwa akitakiwa na
bendi ya Mashujaa kwa dau zuri, lakini amekuwa akikataa kutokana na jinsi
anavyomheshimu Asha Baraka, lakini anasikitika amefukuzwa kwa kudhalilishwa.
“Amenikfukuza na kunitolea maneno ya kashfa mimi wakati nipo
na bendi yake ziarani mikoani, imeniuma sana. Ila bado nitaendelea kumuheshimu
Asha Baraka kama dada yangu na mtu ambaye amenifikisha hapa.”alisema Martine.
Sababu kubwa aliyoitaja Asha ya kumfukuza Martine ni
kuwarubuni wanamuziki wa Twanga Pepeta kuhamia kwa wapinzani, Mashujaa. Miongoni
mwa wanamuziki wa Twanga waliohamia Mashujaa ni mwimbaji hodari, Charles Baba.
0 comments:
Post a Comment