Shearer wa sasa |
WAKATI michuano ya Euro 2012 iko njiani, ikiwa inaanza mwezi ujao- wapo baadhi ya magwiji waliong'ara kwenye fainali zilizopita za michuano hiyo na kuingia kwenye vitabu vya kumbukumbu za kudumu.
Mmojawao ni Alan Shearer Alan aliyezaliwa Agosti 13, 1970, ambaye amecheza soka
katika ngazi ya juu katika ligi ya England kwa klabu tofauti ambazo ni
Southampton, Blackburn Rovers, Newcastle United na pia timu ya taifa ya
England.
Shearer enzi zake na jezi ya Three Lions |
Anatambulika kama mshambuliaji bora wa England akiwa pia
mfungaji bora anayeshikilia rekodi katika klabu ya Newcastle na Ligi Kuu
England. Baada ya kustaafu mpira, Shearer sasa anafanya kazi kama mchambuzi wa
soka katika Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC). Wakati anakaribia
kustaafu uchezaji soka, Shearer alijitahidi kupata leseni ya ukocha
inayotambulika kama UEFA Pro License, na kueleza nia yake ya kuwa meneja. Mwaka
2009, aliacha kwa muda jukumu lake BBC ili kuwa meneja wa timu ya Newcastle
United katika mechi zake nane za mwisho wa msimu wa 2008–09 lakini akashindwa
kuiepusha isishuke daraja.
Akiwa mzaliwa wa Newcastle, Shearer alianza kucheza soka la
kulipwa mwaka 1988 katika klabu ya Southampton ambapo katika mchezo wake wa
kwanza alifunga mabao matatu maarufu kama hat-trick. Alijijengea heshima kwa
uchezaji wake ambao ulikuwa unatumia nguvu na uwezo wa kufunga mabao ambapo
ilimwezesha kuitwa timu ya taifa pamoja na kuhamia timu ya Blackburn Rovers mwaka
1992. Shearer alikuwa mchezaji muhimu katika timu ya taifa ya England na mabao
yake 34 yaliiwezesha Blackburn kushinda taji la Ligi Kuu England msimu wa
1994–95. Alichaguliwa Mchezaji Bora na Chama cha Waandishi England mwaka 1994
na akashinda tuzo ya Mchezaji Bora mwaka 1995. Msimu wa 1995–96, ulishuhudia
Shearer akicheza kwa mara ya kwanza Ligi ya Mabingwa na kumaliza mfungaji bora
wa Ligi Kuu na mabao 31. Pia alikuwa mfungaji bora katika Kombe la Ulaya 1996
akiwa na timu ya taifa ya England, ambapo alifunga mabao matano, na akawa
mfungaji wa Ligi Kuu England msimu 1996–97 akifunga mabao 25.
Baadaye alihamia katika timu aliyokuwa anaipenda tangu
utotoni ya Newcastle United baada ya mafanikio ya Euro ’96 kwa kitita
kilichovunja rekodi wakati huo cha paundi milioni 15 ambapo aliichezea timu
hiyo hadi anastaafu. Ingawa alishindwa kupata mafanikio kama aliyokuwa nayo
Blackburn Rovers, Shearer alipata tuzo ya mshindi wa pili katika Ligi Kuu na
Kombe la FA, na tuzo yake ya pili ya Mchezaji Bora Ligi Kuu. Baada ya
kuchaguliwa nahodha wa timu taifa ya England mwaka 1996 na nahodha wa Newcastle
mwaka 1999, alistaafu soka la kimataifa baada ya Euro 2000, ambapo alicheza
mechi 63 na kufunga mabao 30 kwa timu nchi yake.
Shearer alizaliwa Gosforth, Newcastle mwaka wa 1970 ambapo
wazazi wake Alan na Anne Shearer walikuwa wachapakazi. Shearer alishauriwa na
baba yake kucheza mpira akiwa na umri mdogo nay eye aliendelea hata akiwa
shule. Alisoma katika shule ya Gosforth Central Middle na Gosforth High School.
Wakati anakuwa kisoka, alipenda kucheza nafasi ya kiungo kwasababu aliona ndiyo
inayomfanya aonekane kucheza.
Shearer alikuwa nahodha wa timu yake ya shule na pia
kuisaidia timu ya Newcastle City Schools kushinda taji ya wachezaji saba kila
upande katika mashindano yaliyofanyika St James' Park. Badaye alijiunga na
Wallsend Boys Club akiwa chipukizi. Wakati anaichezea timu hii, alionekana na
skauti kutoka Southampton anayejulikana kama Jack Hixon, ambapo Shearer alikuwa
nafanya mazoezi na timu yao ya vijana wakati wa majira ya joto. Shearer alifuzu
majaribio katika klabu za daraja la kwanza ambazo ni West Bromwich Albion,
Manchester City na Newcastle United, kabla ya kupewa mkataba ya vijana na timu
ya Southampton, April mwaka 1986.
Baada ya msimu miwili akiwa na timu ya vijana, Shearer
alipandishwa hadi kuchezea timu ya kwanza. Mechi yake ya kwanza akiwa mchezaji
wa Southampton ilikuwa Machi 26, 1988 akiingia kama mchezaji wa akiba katika
mechi ya Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya Chelsea.
Wiki mbili baadaye, alikuwa katika kikosi cha kwanza katika
mechi dhidi ya Arsenal na kufunga hat-trick katika ushindi wa mabao 4-2 na
hivyo basi kuvunja rekodi ya miaka 30 iliyowekwa na Jimmy Greaves ya mchezaji
chipukizi kufunga hat-trick katika ligi ya juu. Wakati anafunga hat-trick, Shearer
alikuwa na miaka 17 na siku 240. Shearer alimaliza msimu wa 1987–88 na mabo
matatu katika michezo mitano na kuzawadiwa mkataba wake wa kwanza wa soka la
kulipwa.
Kutoka Southampton, Shearer alihamia Blackburn Rovers ambapo
aliichezwea kuanzia mwaka 1992 hadi 1996. Ingawa bosi wa Manchester United,
Alex Ferguson, alimtaka Shearer, alizidiwa kete, ujanja na fedha za mdhamini wa
Blackburn, Jack Walker, aliyemg'oa mshambuliaji huyo kutoka Saints hadi Ewood
Park katika majira ya joto ya 1992.
Msimu wake wa kwanza ulikuwa wa maajabu kwani alikosa nusu
ya msimu huo kutokana na kuwa majeruhi wakati wa mechi dhidi ya Leeds, lakini
alifunga mabao 16 katika michezo 21 alizocheza. Shearer pia alikuwa mchezaaji
wa kutegemewa katika timu ya taifa ya England msimu huo kwani alifunga bao lake
la pili la kimataifa katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 1994 wakati wa
ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Uturuki.
Shearer baadaye alihamia timu ya Newcastle United kuanzia
1996 hadi 2006 alipostaafu soka. Baada ya Euro 96, Manchester United kwa mara
nyingine tena waliitafuta kwa udi na uvumba saini ya Shearer. Mshambuliaji huyo
anakiri kuwa nusura ajiunge na Mashetani Wekundu baada ya mazungumzo marefu na
meneja wa Man United, Alex Ferguson. Hata hivyo, mmliki wa Blackburn Rovers, Jack
Walker, aligoma kumuuza Shearer. Baadaye Manchester United pamoja na Newcastle
United walikubaliana ada ya uhamisho na Blackburn Rovers, ambapo Shearer
alikuwa tayari kujiunga na Manchester United lakini katika dakika ya mwisho
Kevin Keegan aliomba kukutana na Shearer na kumshawishi kuwa maisha yake yapo
St. James Park. Julai 30 mwaka 1996, Shearer alijiunga na timu yake ya utotoni
ambayo ilikuwa ikifundishwa na mtu aliyekuwa anamhusudu; Kevin Keegan.
Shearer alichezea mechi yake ya kwanza akiwa na jezi ya
Newcastle Agosti 17, 1996 dhidi ya Everton, na kuendeleza utikisaji wake wa
nyavu ambapo alimaliza mfungaji bora wa Ligi Kuu England kwa msimu wa tatu
mfululizo. Hata hivyo taji la Ligi Kuu England ilikuwa taabu kwa Newcastle
kupata ambapo walimaliza katika nafasi ya pili mfululizo na kupelekea Keegan
kubwaga manyanga.
Tangu amestaafu soka, wametokea washambuliaji wengi England, wakiwemo wa sasa akina Wayne Rooney, lakini bado inaaminika hajatokea wa kufikia makali ya mkali huyu wa mabao. Labda tusubiri siku zijazo, atatokea wa kumpiku Shearer, ila kwa sasa bado.
Shearer wa Newcastle |
WASIFU WAKE:
JINA: Alan Shearer Alan
KUZALIWA: 13 Agosti 1970 (Miaka 40)
ALIPOZALIWA: Gosforth, Newcastle, England
KLABU ALIZOCHEZEA:
Mwaka Klabu
1988–1992 Southampton
(Mechi 118, mabao 23)
1992–1996 Blackburn
Rovers (Mechi 138, mabao 112)
1996–2006 Newcastle
United (Mechi 303, mabao 148)
(Tangu 1992 hadi 2000, ameichezea England mechi 63,
ameifungia mabao 30)
0 comments:
Post a Comment