Muntari |
KLABU ya Juventus uongozi wake katika Ligi Kuu Italia, Serie A dhidi ya mabingwa watetezi, AC Milan umepunguzwa hadi kubaki tofauti ya pointi moja baada ya makosa ya kipa Gianluigi Buffon kuwafanya wafungwe bao la kizembe dakika za lala salama na kutoka sare ya 1-1 na Lecce.
Buffon alikuwa 'anaremba' bila ya kujua Andrea Bertolacci, alikuwa anamuwinda na akaupitia mpira na kumpiga chenga kisha kuutumbukiza kwenye nyavu langoni kukiwa hakuna mtu dakika ya 85. Buffon kwa kosa hilo, aliinua mikono yake kuwaomba radhi mashabiki na wachezaji wenzake.
Claudio Marchisio alitangulia kufungia mapema tu Juventus, iliyocheza kwa faida ya mchezaji mmoja zaidi uwanjani baada ya Juan Cuadrado kutolewa nje dakika ya 55 alipoonyeshwa kadi ya pili ya njano.
AC Milan iliwafunga wageni Atalanta 2-0, mabao ya Sulley Muntari dakika ya tisa na Robinho dakika ya 90.
Juventus iliyoshinda mechi 22 na sare 14, ikiwa haijafungwa hata mechi moja inajaribu kuweka rekodi ya kuchukua ubingwa wa Serie A bila kufungwa tangu AC Milan ilipoweka rekodi ya kushinda mechi 22 na sare 12 bila kufungwa msimu wa 1991-92.
0 comments:
Post a Comment