Guardiola

MAN CITY BADO WANAYE TU VAN PERSIE

KLABU ya Manchester City wako mstari wa mbele katika kuwania saini ya mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi, Robin Van Persie, mwenye umri wa miaka 28, ikiwa Arsenal watalazimika kumuuza mpachika mabao huyo nyota.
MABINGWA wa England, Manchester City wanaongoza mbio za kumuwania nyota wa Sunderland, Stephane Sessegnon, mwenye umri wa miaka 27, na wana nafasi nzuri ya kumng'oa Stadium of Light.
MPANGO wa Fabio da Silva, mwenye umri wa miaka 21, kwenda kucheza kwa mkopo Benfica umeingia zengwe — baada ya QPR nao kuibuka wakimtaka beki huyo wa Manchester United.
KLABU za Arsenal, Tottenham na QPR wote wanapigana vikumbo kuwania saini ya mkongwe Alessandro Del Piero, mwenye umri wa miaka 37, ambaye amesema hataki kuendelea kucheza Serie A.
Leandro Damiao
Leandro Damiao.
KLABU ya Tottenham Hotspur iliweka mezani dau la pauni Milioni 14 ili kumnasa mshambuliaji wa Internacional, Leandro Damiao, mwenye umri wa miaka 22, ambalo hata hivyo lilikataliwa na kocha Harry Redknapp anatarajiwa kuongeza, katika jitihada za kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.
BEKI wa Arsenal, Bacary Sagna ameiambia klabu yake imsajili Mfaransa mwenzake,  Yann M'Vila, mwenye umri wa miaka 21, kama inataka mshambuliaji wao nyota, Robin van Persie asiondoke.

GUARDIOLA ANUKIA CHELOTHER GOSSIP

KOCHA wa Muda wa Chelsea, Roberto Di Matteo ameibuka kama mtu namba moja anayefikiriwa kupewa mikoba ya ukocha wa klabu ya Aston Villa.
Roberto Di Matteo
Roberto Di Matteo.
Di Matteo na Msaidizi wake, Eddie Newton, wamewekwa kizani juu ya mustakabali wao Chelsea, baada ya klabu hiyo kuanza rasmi mpango wa kumuhamishia kocha Pep Guardiola aliyejiuzulu Barcelona, kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.
MMILIKI wa Chelsea, Roman Abramovich anafanya pilika za kumtwaa Guardiola akapige kazi Magharibi mwa London, lakini jitihada zake zinakabiliwa na upinzani kutoka kwa Manchester United, ambao nao pia wanamtaka.
KOCHA Sir Alex Ferguson hafikirii mustakabali wake kama kocha wa Manchester United, licha ya maneno ya Mwenyekiti wa Wigan, Dave Whelan kwamba babu huyo mwenye umri wa miaka 70 atastaafu msimu ujao, kufuatia matatizo ya kiafya wiki iliyopita.
KLABU ya Liverpool imepiga hatua kubwa katika harakati zake za kumtwaa Louis van Gaal kama Mkurugenzi wa Michezo, kufuatia kukutana naye nchini Ureno wiki iliyopita.

MICHAEL OWEN KUTUA WEST HAM.

NYOTA wa zamani wa West Ham, Tony Cottee amewataka The Hammers kubomoa benki yao na kumsajili mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa England, Michael Owen ambaye kwa sasa ni mchezaji huru.