Beki wa Yanga, Chacha Marwa |
MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Polisi Dodoma
iliyochezwa (Aprili 22 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
ilishuhudiwa na watazamaji 1,635 na kuingiza Sh. 5,666,000.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace
Wambura Mgoyo amesema kwamba, baada ya
kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) ambayo ni Sh. 864,305.08 kila klabu ilipata sh. 193,858.47,
uwanja sh. 26,469.49.
Wambura alisema TFF ilipata Sh. 26,469.49, Chama cha Mpira
wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 108,687.80. Mfuko wa Maendeleo ya
Mpira wa Miguu (FDF) sh. 13,234.75, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh.
2,646.95 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 26,469.49.
Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa
waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. Mwamuzi
wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa kamishna na waamuzi sh. 160,000,
gharama ya tiketi sh. 1,500,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 1,500,000 na
Wachina (Beijing Construction) sh. 1,000,000.
Kutokana na mechi hiyo kuingiza kiasi kidogo baadhi ya
gharama zililipwa nusu au kutolipwa kabisa na kuacha madeni. Madeni hayo ni
tiketi sh. 1,500,000, maandalizi ya uwanja (pitch marking) sh. 400,000, umeme
sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 850,000 na Wachina sh. 1,000,000.
0 comments:
Post a Comment