Yanga SC, mechi inayo na Simba |
YANGA, imekumbuka shuka, wakati kumekucha baada ya jana
kuichapa JKT Oljoro mabao 4-1, katikamchezo
Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid,
mjini Arusha.
Kwa matokeo hayo, Yanga imeweza kufikisha pointi 49 huku
ikiendelea kushika nafasi ya tatu, baada ya Azam kufikisha pointi 50 inayoshika
nafasi ya pili, wakati Simba inaongoza kwa pointi 59.
Yanga ambao walikuwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo,
imelitema kombe hilo, baada kuboronga mechi mbili huku ikinyang'anywa pointi
tatu na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania.
Kamati hiyo, ilichukua uamuzi huo, baada ya Yanga
kumchezesha, Nadir Haroub 'Cannavaro' katika mechi yao dhidi ya Coastal Union,
iliyochezwa Machi 31, kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Yanga ilimtumia mchezaji huyu ambaye alikuwa anatumikia
adhabu ya kadi nyekudu kutokana na kumshambulia mwamuzi Israel Nkongo,
aliyechezesha mechi yao dhidi ya Azam, Machi 10, mwaka huu, Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Hata hivyo, matarajio ya Yanga kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya Afrika
mwakani ni finyu, kwani imesaliwa na mechi moja dhidi ya Simba itakayochezwa
Mei 5, mwaka huu, Uwanja wa Taifa.
Katika mechi hiyo, Yanga ikishinda itafikisha pointi 52,
ambapo Azam itakuwa na uwezo wa kufikisha pointi 56 iwapo itashinda michezo
miwili dhidi ya Toto African na Kagera Sugar, huku ikisubiri hatma ya matokeo
ya mechi yao dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo
juzi ulivunjika kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Mechi hiyo, ilivunjika
baada ya timu hizo kufunga bao 1-1, lakini mwamuzi wa mchezo huo Rashid
Msangi kutoka Dodoma, alivunja pambano hilo, kwa madai Mtibwa waligomea
penelti..
Katika mchezo wa
kwanza uliochezwa kwenye
Katika mchezo huo wa jana,
Yanga iliandika bao dakika ya 36
likifungwa na Hamisi Kiiza, kabla ya Haruna Niyonzima kufunga la pili dakika 40.
Yanga ikicheza bila Kocha mkuu wake, Kostadin Papic, Kiiza
alifunga bao la tatu ikiwa ni dakika moja kabla ya kwenda mapumziko ambapo Pius
Kisambale akihitimisha 'sinia' la mabao katika dakika 84.
Bao la kufutia mafunzo la JKT Oljoro lilifungwa na kwa njia
ya penelti.
Ligi hiyo, inatarajia kuendelea leo kwenye Uwanja wa
Chamazi, Dar es Salaam, kwa timu ya Azam itakapoivaana na Toto African.
0 comments:
Post a Comment