MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kati ya wenyeji
Coastal Union na Yanga ya Dar es Salaam iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Mkwakwani, mjini Tanga,
imeingiza kiasi cha Sh. 61,494,000 kutokana na mashabiki 11,056 waliokata tiketi
kushuhudia pambano hilo.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzsania (TFF),
Boniphace Wambura Mgoyo, amesema leo, pamoja na kupatikana kwa kiwango hicho, kila
timu ilipata Sh. 14,664,927.80.Wambura alisema katika mechi hiyo, viingilio vilikuwa Sh. 10,000 kwa VIP, Sh. 6,000 jukwaa kuu na Sh. 4,000 mzunguko na mbali na mgawo wa timu na gharama za awali za mchezo, fedha nyingine asilimia 18 ililipiwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), Uwanja Sh. 4,630,335.93 na Chama cha Soka Tanga (TRFA) Sh. 2,515,494.37,
TFF Sh. 4,630,335.93, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) Sh. 2,315,167.97 na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Sh. 463,033.59.
Aidha, mechi kati ya African Lyon na Simba iliyochezwa Machi 31 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza Sh. 29,716,000 kutokana na watazamaji 8,167 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo na baada ya kuondoa asilimia 18 ya VAT (Sh. 4,532,949.15) kila timu ilipata sh. 5,031,085.25.
Uwanja ulilipiwa Sh. 1,486,465.08, TFF ilijikatia Sh. 1,486,465.08, Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA) Sh. 1,084,600.03, FDF Sh. 743,232.54 na BMT Sh. 148,646.51.
Mechi nyingine ya Ligi Kuu kati ya Azam na Ruvu Stars Aprili 1, mwaka huu Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam imeingiza Sh. 1,585,000.
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kila timu ilipata sh. 283,656, uwanja sh. 57,942, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 117,306.08, TFF sh. 57,942, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 28,971 na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 5,794.02.
Wakati huo huo: Rais wa TFF, Leodegar Tenga amekataa barua ya kuomba kujiuzulu ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi ya TFF, Said Mohamed.
Mohamed ambaye ni Mwenyekiti wa klabu ya Azam alimuandikia Rais Tenga barua ya kujiuzulu wadhifa huo akipinga kauli ya Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Alfred Tibaigana juu ya adhabu zilizotolewa na Kamati ya Ligi kwa baadhi ya wachezaji wa Yanga.
Rais Tenga amesema alimteua Mohamed katika Kamati hiyo kwa kuzingatia uadilifu wake na uwezo wake katika kuongoza, hivyo amekataa barua hiyo ya kuomba kujiuzulu.
Kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa na Mkutano Mkuu wa TFF, Rais Tenga, Oktoba 28 mwaka jana aliunda Kamati ya Ligi ambayo wajumbe wake wanatoka kwenye klabu za Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza.
Wajumbe wa kamati hiyo ni Wallace Karia (Mwenyekiti), Said Mohamed (Makamu Mwenyekiti), Damas Ndumbaro, Steven Mnguto, Geoffrey Nyange, Seif Ahmed, Henry Kabera, ACP Ahmed Msangi, Meja Charles Mbuge na Ahmed Yahya.
0 comments:
Post a Comment