LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaingia raundi yake ya 25
na kesho (Aprili 25 mwaka huu) Oljoro JKT itaikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha wakati JKT Ruvu itakuwa
mwenyeji wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace
Wambura Mgoyo amesema kwamba Raundi hiyo itakamilika kwa mechi nne; Aprili 28
mwaka huu Coastal Union itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga huku Mtibwa Sugar ikiwa mgeni wa African Lyon kwenye
Uwanja wa Chamazi.
Alisema Azam na Toto African zitacheza Chamazi, Aprili 30
mwaka huu wakati Mei 1 mwaka huu Villa Squad itaumana na Oljoro JKT kwenye
Uwanja wa Chamazi.
Ligi hiyo itafunga msimu wa 2011/2012, Mei 5 mwaka huu
ambapo timu zote 14 zitakuwa uwanjani. Simba vs Yanga (Uwanja wa Taifa), Oljoro
JKT vs Polisi Dodoma (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha) na Ruvu Shooting vs
Villa Squad (Mabatini, Mlandizi).
Mechi nyingine zitakuwa kati ya Coastal Union vs Toto
African (Mkwakwani, Tanga), African Lyon vs JKT Ruvu (Manungu, Morogoro), Azam
vs Kagera Sugar (Chamazi, Dar es Salaam) na Moro United vs Mtibwa Sugar
(Jamhuri, Morogoro).
Wakati huo huo: Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesigwa amesema kocha Kostadin Papic ahajaenda na timu Arusha.
Mwesigwa hakutaka kuzungumzia kwa undani sakata hilo, lakini habari ambazo bongostaz.blogspot.com inazo ni kwamba kocha huyo anashinikiza apewe mkataba mpya.
0 comments:
Post a Comment