Wilshere |
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger
amesema kwamba wiki tatu zijazo zitaamua kama Jack Wilshere atacheza msimu huu.
Kiungo huyo wa England hajachezea
kikosi cha kwanza cha Arsenal tangu majira ya joto msimu uliopita baada ya
Kombe la Emirates alipokwenda kufanyiwa upasuaji Septemba.
Wilshere anaendelea vizuri na maumivu
yake, lakini Wenger amesema hataki kucheza ‘kamari’ juu ya ufiti wa mchezaji
huyo.
"Tutajua katika wiki mbili
au tatu zijazo [kama atacheza msimu huu]," alisema kocha huyo. Wilshere alikwishakamata namba kwenye kikosi
cha England msimu uliopita, lakini bado anatazamiwa hali yake kama atakuwa
tayari katika kikosi cha nchi hiyo kitakachokwenda kwenye Kombe la Mataifa ya
Ulaya, Euro 2012 Juni, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment