Taarabat akishangilia bao lake |
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger anaamini kiungo wa QPR, Adel
Taarabt ana kila kitu cha kuitwa mchezaji bora – lakini kwa sasa anahitaji kuw
amwendelezo wa kufanya mavituz uwanjani kila wiki.
Taarabt aliilipua Arsenal Jumamosi kwa bao lake la kuongoza
aliloifungia QPR ikishinda 2-1 kwenye Uwanja wa Loftus Road – hilo likiwa bao
lake la kwanza katika Ligi Kuu msimu huu.Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Morocco, alikuwa chachu ya timu yake kupanda Ligi Kuu msimu uliopita, akiifungia mabao 19 na Wenger amesema kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 sasa anatakiwa kudumisha ubora wake uwanjani.
“Ni mwanasoka mwenye kipaji sana,” alisema kocha wa Arsenal. “Ameonyesha hapa kwamba ana kipaji, hilo nilijua.lakini anatakiwa kufanya mavituz kama hayo katika kiwango cha mfululizo.
“Hapana (sijawahi kujaribu kutaka kumsajili). Alikuwa Lens na kasha akaenda Tottenham. Ni mchezaji mzuri na mwenye hamasa, lakini anatakiwa kufanya hivyo kila wiki.”
0 comments:
Post a Comment