Viongozi washtukia janja ya wazee Yanga Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 28th April 2012 @ 14:50 Imesomwa na watu: 91; Jumla ya maoni: 0
|
|
Makao makuu ya Yanga jijini Dar es Salaam. |
|
|
|
WAZEE wa klabu ya Yanga waliokuwa wakitaka kuiteka timu hiyo, wamekwama.
Taarifa za wazee hao kuiteka timu hiyo zilizagaa mapema jana ambapo ilidaiwa kuwa wazee hao waliitaka timu ili waifanyie maandalizi ya mechi dhidi ya watani wao wa jadi, Simba, inayotarajiwa kuchezwa Mei 5 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Taarifa zilizopatikana jijini jana zilisema wazee hao wakiongozwa na Katibu wao, Ibrahim Akilimali walidai kwa baadhi ya wajumbe wa Yanga kwamba waliruhusiwa kufanya hivyo na Mwenyekiti Lloyd Nchunga.
Akizungumza Dar es Salaam jana, mmoja wa wajumbe wa kamati ya Utendaji ya Yanga, Mohamed Bhinda alikiri kutokea kitu hicho lakini wazee walishindwa kutimiza azma yao baada ya yeye (Bhinda) kuwasiliana na mwenyekiti wao.
Bhinda alisema ni kweli wazee hao walimfuata na kumwambia wanataka timu baada ya kuambiwa na mwenyekiti wa Yanga, ndipo alipoamua kuwasiliana nae na kumwambia taarifa hizo si za kweli.
"Ni kweli wakati tupo kwenye kikao na wachezaji wazee walikuja na kusema kuwa wanataka timu wameambiwa na mwenyekiti lakini baada ya kuwasiliana na mwenyekiti, akaniambia hakuna kitu kama hicho," alisema.
Bhinda alisema mpaka jana mchana kamati ya Utendaji ilikuwa kwenye kikao lakini baadhi ya mambo yaliyoamuliwa ni kwamba wachezaji wote wamerudi majumbani mwao mpaka kesho asubuhi katika mazoezi na ndipo watajua waweke wapi kambi kwa ajili ya maandalizi na mechi yao dhidi ya Simba.
Yanga imeingia kwenye mgogoro baada ya kupoteza ubingwa na pia kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa, kutokana na hilo, baadhi ya wajumbe wa kamati ya Utendaji wamejiuzulu.
Yanga ambayo inashikilia pia ubingwa wa soka Afrika Mashariki na Kati, iko nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 49 ikiwa nyuma ya Azam yenye pointi 53 na Simba inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 59.
|
|
|
|
|
0 comments:
Post a Comment