CHAMA cha Riadha Kenya kimetangaza orodha ya wanariadha watakaowakilisha Kenya katika michezo ya Olimpiki ya mjini London baadaye mwaka huu.
Miongoni mwa waliotajwa ni Wilson Kiplagat ambaye alishinda mbio za Marathon ya mji wa London siku ya Jumapili iliyopita na mshindi wa mara mbili wa mashindano ya dunia Abel Kirui pamoja na Moses Mosop aliyemaliza wa tatu kwenye mbio za Rotterdam mwezi huu.
Hata hivyo Patrick Makau anayeshikilia rekodi ya dunia ametupwa nje baada ya kushindwa kumaliza mbio za London Marathon siku ya Jumapili.
Kwa upande wa wanawake, washindi waliochukua nafasi tatu za mwanzo katika mbio za London Marathon Mary Keitany, mshindi wa dunia Edna Kiplagat na Priscah Jeptoo wamechaguliwa kuiwakilisha Kenya katika mashindano ya Olimpiki ya London mwaka 2012.
0 comments:
Post a Comment