Na
Baraka Mbolembole
Aliyekuwa
kocha watimu ya taifa ya Brazil, Luiz Fillipe Scolari alimuita mshambuliaji
Ronaldo De Lima katika kikosi cha ‘Selecao’ kwa ajili ya michuano ya kombe la
dunia mwaka 2002 katika nchi za Korea Kusini na Japan. Uamuzi wake huo
uliwagawa Wabrazil wengi ambao hawakuona kama Ronaldo angewasaidia, Ronaldo
ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa miaka miwili kutokana na majeraha alionekana
si kitu mbele ya Wabrazil ambao walitaka nyota Romario De Souza ndiye angeitwa.
Utata ambao uliishia kwa mashabiki wenye hasira wa Brazil kumzingira kocha huo
siku ya mwisho baada ya kutaja majina ya wachezaji 23 wa ‘Selecao’, mashabiki
hao ambao ilisemekana walikuwa wakitaka kuteka kocha huyo walitawanywa haraka
na jeshi la polisi.Aliyekuwa Rais wa Brazil, Lula Da Silva wakati huo naye aliingia katika mkumbo wa kumponda Ronaldo na kumtaka kocha kumjumuhisha Romario na si Ronaldo. Unajua Scolari alimjibu nini Rais wan chi yake? ‘ Tupishe mimi na Ronaldo katika nafasi yako, na umchukue Romario uende ukaifundishe wewe Brazil kwa mwezi mmoja’. Matokeo ya mwisho ilikuwa ni Brazil kutwaa taji pale, Yokohama,uku Ronaldo akiibukas mfungaji bora wa michuano hiyo. Miaka mine baadae Wabrazil wakiongozwa na wachezaji nyota wa zamani wan chi hiyo, rais wa nchini Lula Da Silva, Pele, Tostao waliponda wazi uwepo na Ronaldo katika kikosi cha Brazil mwaka 2006 katika michuano ya kombe la dunia. Ronaldo ambaye alikuwa katika umbo ‘nene’ alikuwa na msimu mbaya katika klabu yake ya Real Madrid. Kocha wa Brazil wakati huo Carlos Alerto Perreira alimjumuhisha kikosini japo wengi walimuona ‘mpumbavu’.
Katika mchezo wao ewa ufunguzi wa kombe la dunia mwaka 2006 dhidi ya Croatia ambayo Brazil ilishinda kwa tabu, baada ya bao la ‘video’ la Ricardo Kaka’, Ronaldo alitajwa na vyombo vya habari vya kwao kuwa ndiye alikuwa mchezaji ‘mchovu’ zaidi katika kikosi cha Brazil siku hiyo. KIWANGO KIBOVU ALICHOKIONESHA KATIKA MCHEZO HUO KWA ZAIDI YA DAKIKA 65 ALIZOKUWEMO UWANJANI SIKU HIYO ZILIMFANYA Perreira kumtoa na kumuingiza Robinho ambaye alikuwa akiitwa ‘Pele Mpya’ wakati huo (2006). Mshambiaji nyota wa zamani wa Brazil, Tostao ambaye ni mwandishi anayeheshimika nchini humo, aliandika katika gazeti la Folha “ brazil ilikuwa ikicheza taratibu na ‘kizembe’, tena bila mpangilio, ilikuja kuzinduka baada ya Robinho kumbalidi Ronaldo ambaye alikuwa akicheza taratibu na kizembe. Kitu chga kusifu ni kwamba Brazil iliifunga Croatia ikiwa na wachezaji 10, ama 9’ tostao alikuwa ikipondonda kiwango cha chini cha Ronaldo na patna wake Adriano Leite.
‘Ilikuwa ni udhalilishaji kumuacha Ronaldo akiendelea kucheza. KOcha Perreira alipaswa kumtoa ili kumlindia heshima yake. Ilikuwa aibu kumuona akizunguka zunguka uwanjani kama bonge ‘nyanya’ aliyevamia uwanja wa mchezo ambao hauusiani naye’ aliwahi kuandika, Tostao akimponda Ronaldo. Pias mwandishi maarufu wa safu za micvhezo nchini humo humo Fernando Calazan naye aliandika na kumshutumu Ronaldo. ‘ Wawili hao walionekana kama waliokwenda kufanya matembezi bustanini. Ajabu ni kwamba walikuwa pamoja uwanjani kwa dakika 69. Matokeo yake mipira ikawa inawagonga Ronaldo na Adriano na kurudi nyuma, mpira ukawa haukai mbele kwa zaidi ya sekunde tano, jambo ambalo liliwapa mzigo zaidi mabeki.
RONALDO ALIWAJIBU TENA KAMA ALIVYOFANYA KOREA, JAPAN, NI VITENDO TU UWANJANI
Baada ya kupondwa kama ilivyokuwa wakati akienda katika fainali za barani Asia mwaka 2002, kwea kuibuka ,mfungaji bora wa michuano hiyo. Ronaldo alitumia mechi dhidi ya Japan kuifikia rekodi iliyokuwa imewekwa na Gerd Muiller wa Ujerumani kama mfungaji bora wa muda wote wa michuano hiyo (kumbuka Pele alishindwa kuifikia reko hii japo alicheza mara tatu michuano hiyo). Ronaldo aliibuka kwa mara ya kwanza na kuongea na vyombo vya habari akiwa mwenye furaha baada ya kumalizika kwa mchezo huo, alisema ‘ Nina furaha kupata maendeleo mazuri ya kimwili na kiakili wakati wa michuano hii. Utulivu ndiyo siri ya mafanikio. NImefanikiwa kuwa mtulivu katika vipindi vyote vigumu’ yalikuwa ni maneno ya Ronaldo baada ya kushutumiwa sana na Wabrazil.
Kocha Perreira ambaye ndiye alimuita kwa mara ya kwanza Ronaldo katika timu ya Brazil mwaka 1994 akiwa na miaka 17, naye alioneka kufurahia mafanikio ya kijana wake ambaye alimuamini tangu akiwa kinda. ‘ Ronaldo hayuko katika umbo bora, lakini anapiga hatua kewa hatua anarejea katika kasi yake. Nina hakika atazidi kuwa bora kadri michuano inavyoendelea. Daima wote kikosini tuna imani kubwa na Ronaldo. Ni mchezaji wa kipekee’ alisema Perreira. Na kweli siku chache baadae Ronaldo alifunga bao la 15 katika kombe la dunia dhidi ya Ghana katika mchezo wa raundi ya pili, na kuwa mfungaji bora wa muda wote. Ronaldo alifikia mafanikio hayo baada ya kufanya jitihada binafsi kuweza kuwaonesha mashabiki na wale wote waliokuwa wakimponda namna alivyobarikiwa kipaji katika mchezo huu wa soka..
Hivi sasa hapa kwetu gumzo kubwa ni kuamua kustaafu kuichezea timu ya taifa kwamshambuaji namba moja wa Azam FC, John Bocco. Madai makubwa ya Bocco ni kwamba hapati sapoti ya kutosha kutoka kwa mashabiki. Mashabiki wa klabu za Yanga na Simba wamekuwa wakimzomea mara kwa mara mchezaji huyo, hata wakati timu ikifanya mazoezi katika uwanja wa Karume, au ule wa Taifa. Ukweli ulio wazi ni kwamba zaidi ya 98% wanaiingia katika uwanja wa taifa ni wa Simba na Yanga, ndiyo maana mechi zao kule Chamanzi hazina mahudhulio mengi ya mashabiki. Sasa basi hadothi ya Bocco kustaafu kuichezea Stars ni yak wake binafsi lakini kitu kikubwa ni kwamba Bocco hawezi kuzikabili changamoto za soka. Siku Azam FC wakiwa na mshambuaji mwingine ambaye kocha atamuamini kama anavyoaminiwa Bocco ndani ya timu hiyo, bila shaka atatangaza kuondoka ndani ya timu hiyo. Kwani mashabiki wanaweza kumkubali zaidi mwenzake na kuanza kumzomea yeye.
Ni uamuzi wake binafsi ambao hatakiwi kuingiliwa, na miaka 22 tu na wala hajawahi kushinda kikombe chochote cha maana katika maisha yake ya soka. Bocco ana kipaji kizuri sana katika ufungaji, ana shabaha pia, akipiga golini mara tatu lazima kutakuwa na bao hapo. Lakini vyote hivi anavionesha akiwa na Azam FC, kwa nini anashindwa kufanya hivo akiwa na Stars? Nadhani ukubwa wa Stars ni tofauti na ukiwa unachezea Azam, tena ukiwa hujachezea Simba, au Yanga ni ngumu kupata mafanikio ya haraka. Shaaban Nditti anaweza kuwa mfano mzuri alikuwa bora Mtibwa, lakini alishindwa kumudu kelele za mashabiki wa Simba na Yanga akiwa na Stars-hadi alipojiunga na Simba kwa msimu mmoja na kurejea Stars hivi sasa ana miaka sita mfululizo akiwa ndani ya timu hiyo. Nditti amekuwa imara hivi sasa na japo mashabiki wamekuwa wakiomzomea yeye anaonesha uwezo uwanjani na kuwa mchezaji muhimu hadi sasa. Bahati nzuri kwa Bocco ni kwamba anaaminiwa na makocha wote wanaomfundisha, Jan Poulsen wa Stars na Stewart Hall wa klabu yake. Ningependa kumuona tena Bocco akiwa na jezi ya Stars kwa sababu ni mchezaji mzuri na mwenye kipaji kikubwa cha soka. Akiredi afanye kama walivyofanya Ronaldo De Lima, au Nditti wetu. Wataacha tu kuzomea, kwani nao wanahitaji ushindi muda wote, si unajua mashabiki wa Simba na Yanga walivyo. Najua Bocco atakuwa ameshasoma ushauri mbalimbali uliotelewa na waandishi nchini. Nami napenda kumuona akiwa na jezi ya Stars tena na kutufungia mabao tena.
0 comments:
Post a Comment